MKALAMAWAZINDUA CHANJO YA SURUA
Mkuu wa
Wilaya ya Mkalama, Moses Machali amewataka wazazi wilayani Mkalama kuhakikisha
wanapeleka watoto wao katika vituo vya afya kupatiwa chanjo ya Surua la Rubella
ili kuepuka madhara yanayowezajitokeza ikiwa mtoto hatopata huduma hiyo mapema.
Agizo hilo
amelitoa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo iliyofanyika katika hospitali
ya Wilaya ya Mkalama na kushuhudiwa na wakuu mbalimbali wa Idara, watumishi wa
afya pamoja na wananchi walioleta watoto wao kwa ajili ya huduma ya chanjo.
Viongozi wa
serikali wa vijiji hakikisheni mnahamasisha wananchi ili tuweze kufikia lengo
lililowekwa na serikali” amesema DC Machali.
0 Comments