Said Salim Awadh Bakhresa.
KATI ya miaka ya 1960 hadi 1980, mtu kuwa tajiri alionekana
ni hatari kwa taifa, tena mali zake alizimiliki kwa kificho, vinginevyo
angeitwa mhujumu uchumi. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, taratibu sera za
kibepari zinatawala, ujamaa unapewa kisogo.
Mtu kama ni mbunifu, ana nidhamu ya kutofuja pesa na
anafanya kazi sana kwa nini asiwe tajiri? Utandawazi unasaidia ndiyo maana leo
tunaweza kuwatambua mabilionea wakubwa ambao wanastahili pongezi kwa hatua
walizopiga. Tusisahau kuwa wanaibeba nchi kwa ulipaji kodi.
1. SAID BAKHRESA
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh Bakhresa. Jarida la
Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri 40 Afrika kwamba
anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 620 (karibu shilingi trilioni
moja). Hata hivyo, inadaiwa kuwa tabia ya usiri wa Bakhresa inafanya mali zake
zisijulikane sana, ila ni tajiri zaidi ya kiwango hicho.
Ndiye mmiliki wa makampuni ya Bakhresa yanayotoa bidhaa
zenye chapa ya Azam ambazo zinauzwa nchi mbalimbali Afrika. Ana viwanda vya
nafaka na vinywaji, vyombo vya usafiri wa majini, uuzaji wa chakula, bidhaa za
plastiki na kadhalika. Ndiye mmiliki wa Klabu ya Azam FC.
2. GULAM DEWJI
Huyu ni baba wa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji
‘Mo’. Jarida la Forbes mwaka jana lilimtaja kuwa na utajiri wenye thamani ya
dola milioni 560 (karibu shilingi bilioni 900). Mafanikio yake kibiashara
yalianza mwaka 1970. Kiwanda chake cha 21st Century Textiles, kinatajwa kuwa
moja ya viwanda vikubwa vya nguo Afrika.
3. ROSTAM AZIZ
Inadaiwa anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 420
(shilingi bilioni 672). Anamiliki karibu asilimia 40 ya hisa Kampuni ya Vodacom
Tanzania. Ni mmiliki wa Kampuni ya Caspian inayohusika na uchimbaji wa madini
na ukandarasi nchini Tanzania, nchi kadhaa za Afrika na Asia.
4. DK. REGINALD MENGI
Anatajwa kumiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 280
(karibu shilingi bilioni 450). Ni mmiliki wa kundi la makampuni ya IPP,
yanayomiliki vyombo vya habari, viwanda, migodi ya dhahabu, Tanzanite na
kadhalika.
5. ALI MUFURUKI
Utajiri wake unatajwa kuwa na thamani ya dola milioni 110
(shilingi bilioni 176). Ni mmiliki wa kundi la makumpuni ya Infortech
Investment, inayomiliki maduka yanayouza vitu vya rejareja Tanzania na Uganda.
Vilevile ana vitega uchumi vingine.
6. MUSTAFA SABODO
Ni mfayabiashara mkubwa sana nchini anayemwaga mamilioni kwa
misaada. Wakati wa kuanzishwa kwake, aliipa Taasisi ya Mwalimu Nyerere shilingi
milioni 800, akasaidia shilingi milioni 100 katika mradi wa kustawisha mimea
jamii ya kunde. Vilevile alikipa Chadema shilingi milioni 300. Inadaiwa kuwa
utajiri wake unazidi shilingi bilioni 100. Kampuni yake ya Khoja Shia Itnasheri
Jamat (KSIJ), ndiyo yeye tenda ya kujenga maeneo ya maegesho ya magari Posta,
Dar es Salaam, mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 5.6.
7. ABDUL-AZIZ ABOOD
Kiwango chake cha utajiri hakiwekwi sana wazi lakini
anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 10 wanaotikisa nchi kwa sasa. Anamiliki
viwanda kadhaa mkoani Morogoro, vyombo vya habari, Abood Radio na TV. Anamiliki
mabasi ambayo yanafanya safari zake kati ya Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam.
Ni Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM).
8. MICHAEL SHIRIMA
Ni mmiliki mkuu wa Shirika la Ndege la Precision ambalo
linafaya safari zake ndani ya Tanzania pamoja na nchi mbalimbali za Afrika. Ana
asilimia tano ya hisa katika Beki ya I&M (Tanzania), vilevile ni memba
katika bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo yenye thamani ta shilingi bilioni 200.
Hisa zake Precision ni asilimia 42.91.
9. YUSUF MANJI
Kiwango halisi cha utajiri wake bado hakifahamiki lakini
anafahamika kama mmoja wa mabilionea wakubwa nchini Tanzania. Ni mmiliki wa
makampuni ya Quality Group na majengo ya Quality Centre, Quality Plaza na
kadhalika. Ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na utajiri wake umeifaya timu
kutotetereka tangu alipoanza kuiongoza.
10. MOHAMMED DEWJI
Baba yake anashika nafasi ya pili katika orodha hii. Dewji
au Mo kama anavyoitwa na wengi, anatajwa kuwa bilionea nambari moja katika
orodha ya mabilionea vijana Afrika (orodha hiyo tuliitoa wiki iliyopita). Ni
mmiliki wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL) ambayo
inatengeneza faida ya shilingi bilioni 136 kwa mwaka
1 Comments
Why Mo Dewj anakiwa wa kumi wakati Forbes linamtaja kuwa wa kwanza Afrika mashariki na kati Tanzania kutajwa wa Kwanza
ReplyDelete