Follow us

MAOMBI YA LEO NI KUVUNJA CONNECTION ZOTE NA ULIMWENGU WA GIZA.

Tangazo
BWANA YESU atukuzwe.
Leo naomba tuombe maombi ya kuharibu mawasiliano yeyote na ulimwengu wa roho wa giza.
ulimwengu wa roho wa giza kuna majini, mizimu, shetani mwenyewe, wachawi, waganga wa kienyeji, wanajimu, wasoma nyota, wasoma bao na kila mtu aliye upande wa shetani dhidi yako ili kukumaliza au kukuharibia.
Yakobo 4:7 '' Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. ''
Familia moja hapa Dar es salaam ambao ni marafiki zangu sana walitushirikisha jambo moja ambalo ni madhara makubwa yanayoweza kutokea kati ya mtu na ulimwengu wa roho wa giza. familia ile waliajiri msichana wa kazi ambaye ni binti mdogo sana. Hawakumjua huyu binti kama ni wakala wa shetani na kila siku hupeleka kwa wakuu wa giza habari zote kuhusu familia hiyo. ilichukua miezi kadhaa bila kugundulika lakini mtoto mchanga wa ndugu hao akaanza tabia za ajabu ajabu na kulia kusiko kwa kawaida. Mtoto akawa hawataki wazazi wake bali kila siku anataka alale na msichana yule wa kazi. Kwa sababu hawa ndugu wameokoka kwelikweli waliamua kuomba na pia kushirikisha wana maombi wengine ndipo yule msichana wa kazi alipogundulika na kukubali kuhusu kazi yake anayoifanya ya uwakala wa shetani. Binti yule alisema hadi jinsi walivyochukua damu ya mtoto yule mchanga na kuipeleka kuzimu. Wachawi walikuwa katika process ya kumchukua mtoto. Ni hatari sana lakini ashukuriwe MUNGU BABA maana husikia maombi ya watumishi wake na hujibu.
Ashukuriwe BWANA YESU maana
''Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.-Mithali 18:10 ''
Nimefupisha ushuhuda huu ambao una siri nyingi sana za wachawi ambao ni wakuu wa giza na ili kuipata vizuri familia, au mtu binafsi shetani huweka connection na familia hiyo au mtu huyo.
Ili simu iwe hewani ni lazima iwe imeunganishwa katika mnara.
Ukitaka mawasiliano yasiwepo basi ondoa minara ya simu. huo ni mfano mmoja tu katika ile mingi ambayo inawezekana hata wewe unayo.
Lakini MUNGU aliye hai anasema
''Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.-Zaburi 50:15 ''
Kuna watu shetani amepanda mawasiliano yake na wao kupitia nguo wanazovaa ambazo hazijatakaswa.
Kuna watu shetani anawatesa kwa sababu nywele zao bandia ndio mnara wa shetani kuwa na connection nao.
Kuna watu wanateseka kwa sababu katika familia yao kuna mtu anatumika kipepo na kuwaletea uharibifu.
Kuna watu shetani ameweka makazi kwako kwa sababu network yake ipo kwao kwa sababu ya vipodozi wanavyonunua kila siku.
Nakupa siri hizi ili ujue jinsi ya kuombea vitu vyako na ujue jinsi ya kuharibu mawasiliano kati yako na ulimwengu wa roho wa giza.
Mathayo 16:19 ''Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. ''
BWANA YESU ametupa funguo za kufunga mipango ya kipepo na inafungika hakika.
Kuharibu kila jambo la shetani kwetu na linaharibika.
Kuna wadada na wakaka wengi wana waume rohoni au wake wa rohoni ambao ni majini.
majini hayo huwa wanayaona kwenye ndoto yakizini nao na yakivaa sura za watu mbalimbali.
Waume hao au wake hao majini huwazuia kupata wachumba.
Majini hayo kwa watu ni connection na ulimwengu wa roho wa giza kiasi kwamba kila mchumba akija anakimbia kumbe kwa sababu hujavunja mawasiliano na ulimwengu wa roho wa giza.
Kuna watu wanaishi na mapepo na mapepo hayo yamewazuia kupata kazi, kuolewa, kuoa, kupandishwa vyeo na kupata baraka yeyote. mapepo hayo ni mnara kati yao wanadamu hao na ulimwengu wa roho wa giza ambao kazi yake ni kutesa wanadamu.
Inawezekana kuna mtu alichukua nguo yako ya ndani na kumpelekea mganga wa kienyeji ili kukuharibia baraka zao, nguo hiyo imenenewa maneno na kwa maneno hayo kumekuwa na connection kati yako na ulimwengu wa roho wa giza.
Inawezekama kabisa jina lako limetajwa kwenye madhabau za kipepo na kunenewa maneno mabaya ambayo yamekukamata na kukufanya wewe kuwa mali ya ulimwengu wa roho wa giza lakini ashukuriwe BWANA YESU maana jina lake lina nguvu kuliko wachawi wote na waganga wote.
Lakini leo tena sasa nataka tukaombe ili kuvunja connection zote na ulimwengu wa roho wa giza. Nimetumia maandiko mengi kwenye ujumbe huu ili wewe uyatumie maandiko hayo katika maombi yako ya kila siku ukiharibu kila connection kati yako na ulimwengu wa roho wa giza.
Isaya 60:1 ''Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia. ''
Maombi hayo ni kwa kifupi tu ili kukusaidia wewe kuomba kwa kirefu katika kile kinachokuhusu wewe ila hakikisha unavunja mawasiliano yeyote kati yako na ulimwengu wa roho wa giza.
Kama huwa unaenda kwa waganga wa kienyeji acha kuanzia leo maana kwenda kwa waganga wa kienyeji ni kuifuata network ya kipepo ili ije kwako.
Maombi.
JEHOVAH SHALOM MUNGU amani yangu, ninakushukuru BWANA kwa kunilinda na naamini kabisa baada ya maombi haya utaenda kunipa amani yako baada ya wewe MUNGU wangu kufuta connection yeyote kati yangu na ulimwengu wa roho wa giza.
Nisamehe MUNGU wangu kwa kila uovu niliotenda na kuanzia sasa mimi sitatenda tena dhambi yeyote huku nikijua kwamba ile ni dhambi.
Neno lako linasema niinuke na niangaze maana nuru yangu imekuja. Nuru yangu ni BWANA YESU na kwa jina lake BWANA YESU kila connection kati yangu na ulimwengu wa roho wa giza inafutika.
Kwa jina la YESU KRISTO kila mawasiliano kati yangu na ulimwengu wa roho wa giza nayafuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Kama kuna kitu chochote kilichochukuliwa kwangu na kupelekwa kwa wakuu wa giza ili kiwe connection kati yangu na wao,Kwa jina la YESU KRISTO nafuta mawasiliano hayo kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Kama kuna mtu ameniendea kwa waganga, kama kuna mchawi ananipangia mabaya, yote hayo Kwa jina la YESU KRISTO nafuta mawasiliano hayo kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mawasiliano na ulimwengu wa roho wa giza yanafuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila kitu changu chochote ambacho kimekuwa antena ya wachawi kuniona na kunionea, leo natangaza kwa jina la YESU KRISTO ninafuta mawasiliano hayo. ninateketeza antena zote za kichawi zilizopelekea wachawi kujua kila mipango yangu na kuiharibu kabla sijafanikiwa,Kwa jina la YESU KRISTO nafuta mawasiliano hayo kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Imeandikwa nimpinge shetani naye atakimbia hivyo kwa jina la YESU KRISTO ninafuta mawasiliano yote na giza.
Naondoa kila pando la giza na nalitupa kuzimu ili niwe huru sasa. hakuna siri yangu wataijadili wachawi na maadui zangu maana nimeharibu antena zao zote na nimevunja mawasiliano yao yote.
Asante BWANA YESU maana ulikuja ili mimi niwe huru mbali na kuonewa na kila hila za giza.
Naamini leo naanza mwanzo mpya usioingiliwa na mawasiliano ya ulimwengu wa roho wa giza.
Mimi ni wa nuruni maana nuru yangu ni BWANA YESU. Kuanzia leo mimi naongozwa na ROHO wa MUNGU na shetani na watoto wako wote hamtanipata kamwe kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Asante BWANA maana umenitetea na kuniweka huru kupitia damu yako na jina lako takatifu BWANA YESU.
Ni katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi.
AMen Amen.
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.


ni mimi mwinjilist: LAURENT E. MPOMA
UKITAKA MAOMBI ZAIDI PIGA:0763652896, 0714890889

mungu akubariki sana

endelea kufuatilia zaidiingia hapa===>"https://goo.gl/VU8oX0"

Post a Comment

1 Comments

  1. Nimebarikiwa sana na ujumbe huu na maombi haya kupitia kwa jina LA Yesu Kristo nitapata kufunguliwa kutoka kwenye ulimwengu wa roho ya Giza. Asante

    ReplyDelete