MWANDISHI:
EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Sa Yoo
akajikuta akishangilia kwa furaha, ila sura ya Madam Mery ikapoteza furaha, na
kumfanya Eddy naye kupoteza furaha yake.
“Ina maana
hamuniamini au?”
“Phidaya
nina mjua Godwin hawezi kukamatika kiholela kiasi hicho”
Madam Mery
alizungumza kwa msisitizo, huku akiwa amemkazia macho madam Mery
“Jamani
nimemkuta akiwa amelala chini mguuni amepigwa risasi”
“Kwa nini
tubishane twendeni tukamuone”
Sa Yoo
akaanza kukisukuma kitanda cha Eddy huku Phidaya na Madam Mery wakiwa
wametangulia mbele, huku Shamsa akifwata kwa nyuma. Wakatoka kwenye vyumba
hivyo na kwenda nje. Walipo fika kila mmoja akabaki ameduwaa hususani Phidaya
kwa maana Raisi Godwin na Rahab wametoweka eneo hilo
ENDELEA
“Wamekwenda
wapi?”
Phidaya
aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka. Madma Mery akajikuta akikaa chini, huku
nguvu za mwili zikiwa zimemuishia.
“Tuondokeni
eneo hili si salama”
Eddy
alizungumza huku akijaribu kukaa kwenye kitanda, maumivu makali aliyo yapata
kwenye mbavu zake hayakumzuia kabisa kuweza kunyanyuka na kukaa kitako.
“Utataka
kwenda wapi Eddy?”
“Ni bora
nyinyi kuondoka kuliko kuingia mikononi mwa askari”
“Unataka
kusema kwamba…….”
Phidaya
aliuliza huku macho yake akiwa amemtolea Eddy aliye lala kwenye kitanda hicho.
“Ondokeni
eneo hili sio salamaa”
Eddy
alizungumza kwa msisitizo na kuwafanya Shamsa kuelewa maana yake ni nini.
Shamsa kwa haraka akaingia ndani, moja kwa moja akaelekea katika chumba ambacho
walikuwepo. Akachukua mbastola nne zenye magazine zilizo jaa risasi kisha
akatoka nje kwa haraka.
“Inabidi
kuondoka eneo hili sasa hivi”
“Na Eddy?”
“Mimi
mutaniacha hapa, ondokeni”
Taarifa
hiyo, ikauingiza moyo wa Phidaya simanzi kubwa sana, kwa maana hakujua ni
kwanini mume wake amechukua maamuzi kama hayo. Kwa haraka akamfwata Eddy
kitandani na kukumbatiana huku Phidaya machozi yakimwagika, na Eddy machozi
yakimlenga lenga.
“Nitakuwa
salama”
Phidaya
hakujibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuzidi kumwagikwa na machozi, tayari
Shamsa alisha ingia kwenye moja ya gari, ambalo ni mali ya ikulu. Madam Mery na
Sa Yoo nao wote wakaingia ndani ya gari hilo na kumsubiria Phidaya anaye
endelea kumng’ang’ania mume wake.
“Nenda mke
wangu nitakuwa salama”
“Niahidi
hauto kufa?”
“Nakuahidi,
kimbia kabla askari hawajafika hapa”
Phidaya
akamuachia Eddy na kumpiga busu la mdomo, kisha akashuka kwenye ngazi hizo kwa
haraka na kuingia ndani ya gari, Shamsa ambaye tayari alisha lifungua geti hilo
muda alipo kuwa anashuka chini, akakanyaga mafuta ya gari hilo ambalo ni aina
ya Aud 5q lenye sifa ya kuto kuingia risasi na ndio gari ambalo hutembelea
raisi Godwin.
Kipindi gari
hiyo inamalizikia kutoka nje, machozi yakatiririka usoni mwa Eddy ambaye
hakuweza kujumuika katika safari hiyo, kwanza kutokana na mshono wa oparesheni
aliyo fanyiwa jana tu, pili ni kutokana hajulikani kama yeye ndio Eddy, ila
anajulikana kwa jina la Erickson Forrd hii ni kutokana na sura yake.
Hazikupita
hata dakika tano, ving’ora vya gari za polisi pamoja na usalama wa taifa
vikasikika nje ya nyumba ya Eddy. Alicho kifanya Eddy ni kujilaza kitandani
hapo huku machozi yakiendelea kumwagika.
Askari wengi
wenye bunduki mikononi mwao wakaingia ndani humo kwa umakini, wakaanza kukagua
maiti moja baada ya nyingine.
“Erickson”
Eddy
akamuona Manka akimfwata sehemu alipo lala. Taratibu Manka akapiga magoti
chini, na kumbusu Eddy mdomoni.
“Nashukuru
Mungu nimekupata”
Eddy
hakujibu kitu zaidi ya kumwagikwa na machozi usoni mwake. Madaktari wa jeshi
walio fika eneo hilo la tukio, wakamchukua Eddy na kumuingiza kwenye gari ya
wagonjwa, huku akiambatana na Manka ambaye hakuhitaji kumpoteza tena.
Askari walio
baki huku nyuma kazi yao ikwa ni miili ya askari walio pigwa risasi, kati ya
askari ishirini walio fika katika eneo hilo, ni mmoja tu ambaye ni mlinzi wa
raisi Godwin aliye weza kuwa hai japo hali yake ni mbaya
“Muheshimiwa
raisi…..a…me..ch…..u”
Hakumalizia
kitu alicho kuwa anakizungumza akapoteza fahamu.
“Muwahisheni
hospitalini, huyu atatufaa”
Mkuu wa
kitengo cha polisi kanda maalimu bwana Erinest Komba aliwaeleza vijana wake,
ambao wakafwata amri kama alivyo zungumza mkuu wao. Habari ya raisi Godwin
kutoweka ikaanza kusambaa kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii, huku vituo vya
televishion na maredio vikiwa vinatafuta ukweli juu ya jambo hilo. Hapakuwa na
mkuu yoyote wa jeshi aliye weza kudhibitihs habari hizo kwa maana hapakuwa na
mtu mwenye ushahidi katika hilo.
***
“Jikaze
usilie, unavyo lia unadhani mimi nitafanyaje?”
Shamsa
alizungumza huku akimtazama Phidaya anaye lia njia mzima
“Ila mume
wangu atakuwa kwenye matatizo”
“Sio rahisi
kwa Eddy kuingia kwenye matatizo ndio maana akatuambia tuondoke”
Muda wote
madam Mery akawa kimya akilichunguza gari hilo, kwa bahati nzuri akaona kifaa
maalumu ambacho kipo siti ya nyuma ya dereva eneo alilo kaa yeye kinacho weza
kuonyesha ni sehemu gani raisi yupo, hata walinzi wake wanapo kaa ikulu.
“Shamsa
simamisha gari?”
“Kuna nini?”
“Simamisha
gari kwanza”
Shamsa
ikambidi kutii kile kitu ambacho madam Mery amemueleza, kwa haraka madam Mery
akashaka kwenye gari, akamuomba Shamsa kufungua buti ya gari, Shamsa akaminya
batani iliyo ruhusu buti ya gari hilo kufunguka, madam Mery akalinyanyua,
akakuta kifaa kidogo kinacho ongoza kifaa alicho kiona ndani ya gari hilo.
“Ohoo ni
GPRs system”
Sa Yoo
alizungumza mara baada ya kuona kifaa hicho.
“Ndio nini?”
Shamsa
aliuliza mara baada ya kushuka kwenye gari na kuzunguka nyuma kwenye buti ya
gari hilo.
“Sehemu
yoyote tunapo kwenda nah ii gari lazima tuonekane”
“Sasa inakuwaje?”
Hata kabla
Sa Yoo hajajibu swali hilo, wakaziona gari nne nyeusi, aina ya GVC zinazo piga
ving’ora zikiwafwata kwa kasi katika eneo hilo.
“Ohooo
rudini kwenye gari wote”
Shamsa
alizungumza kwa haraka akafunga buti ya gari hilo, wote wakaingia ndani gari,
bila ya kupoteza muda, Shamsa akakanyaga mafuta ya gari na kuondoka eneo hilo
kwa kasi kubwa.
“Fungeni
mikanda”
Shamsa
alizungumza huku akifunga mkanda wa siti aliyo kalia. Gari hizo nne za
makachero wa usalama wa taifa, zikazidi kuifukuza gari hiyo ya raisi huku mkuu
wao aliye panda gari la mbele akiwa na simu maalumu inayo onyesha gari hilo la
raisi kila sehemu anapo kwenda.
“Ongeza
mwendo, hawa watu ndio walio mteka raisi”
“Sawa mkuu”
Dereva huyo,
ambaye naye ni kachero anaye sifika katika maswala ya uendeshaji wa gari kwa
kasi, akawa ndio kama amechochewa, akazidi kukanyaga mafuta kwa kasi, hadi
madereva wezake wanao endesha magri matatu yaliyo nyuma yao akawaacha kwa
umbali kidogo.
“Wanazidi
kutufwata”
Sa Yoo
alizungumza huku mara kwa mara akigeuza kichwa chake nyuma. Katika uendeshaji
wa gari, Shamsa anajimudu sana, ila kitu kinacho mfelisha kwa wakati huu, ni
bega lake lililo pigwa risasi, na ndio kwanza kidonda hakijapona na maumivu
anayo yaoata hapo ni makali kupindukia sema tu anajikaza kuwaokoa wezake kwa
maana wakiingia mikononi mwa Makachero hao, hakuna mtu mwenye jawabu la kujua
ni nini atakacho fanywa.
0 Comments