Follow us

KATIBU WA CCM KATA YA MANDEWA (YUSUPH KIJANGA MAKERA) AKIWA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA MANDEWA

Tangazo

 

  KATIBU WA CCM KATA YA MANDEWA  (YUSUPH KIJANGA MAKERA) AKIWA NA  VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA MANDEWA.

YUSUPH KIJANGA MAKERA

Akiwa na viongozi wenzake kwenye Mkutano Mwaja Kitope, Ni lazima Chama Cha Mapinduzi kiwe na nguvu na kuhamasisha wananchi kukiamini Chama Cha Mapinduzi. Pia alitembelea mradi shule ya chechea iliyopo mwaja kitope na kuhamasisha kwa kuchangia fedha kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa darasa hilo ili kuwezesha watoto wasome na waongezeke ili kupunguza umbali wa kwenda kusoma shule ya msingi mwaja. Na kushirikiana mkuu wa shule ya msingi mwaja kuhakikisha shule ya chechea mwaja kitope hadi kufikia kuwa shule ya msingi.  Alizungumza (KATIBU WA CCM KATA YA MANDEWA).


MWENYEKITI WA MTAA WA MWAJA AKIWA NA KATIBU WA CCM KATA YA MANDEWA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA MANDEWA. 

JOHN PASCALI KIMU

 Tumejitahidi kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi kufikisha umeme mwaja kitope (kamugi) na sasa umeme umewaka imebaki wananchi kuingiza umeme. Pia tulisimamia na tutaendele kusimamia shule ya chechea ya mwaja kitope ili kuhakikisha watoto wanasoma na wanaongezeka ili kuwatoa watoto katika ujinga. Kutokana na maendeleo yanavyoenda kwa kasi katika mtaa wa mwaja sisi viongozi tutajitahidi kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi na wananchi ili kuhakikisha tunapata maendeleo zaidi ya hapa, Kwa kuhakikisha tunapata daraja la kuvuka kwenda malaloni ili kuwasaidia wananchi wanaoishi nga’mbo kwa kupatiwa umeme na barabara hadi kule chuo cha ufundi stadi cha Laurent Vtc Singida. (MWENYEKITI WA MTAA WA MWAJA).

 


KATIBU HAMASA KATA MANDEWA

ANDREA PASCAL KIDINYA

Nimehamasisha watu kujiunga na Chamacha Mapinduzi na tumefanikiwa sana katika eneo hili ndio maana wananchi wanajiunga kwa kasi kubwa kutokana na maendeleo yaliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi yanayoonekana na dira ya Chama Cha Mapinduzi inaelekea wapi. Hivi mwananchi amejiunga na Chama Cha Mapinduzi akitokea Chadema na kupatiwa kadi ya Chama Cha Mapinduzi.

Alizungumza (KATIBU HAMASA KATA MANDEWA).

 

 

 

Post a Comment

0 Comments