MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amechangia mjadala wa hotuba ya Waziri Mkuu ya 2023/2024,na kutoa ombi la kubadili majina ya majimbo ya Singida Mashariki na Singida Magharibi ili kuweka jina lenye utambulisho wa eneo husika.
Akichangia mjadala huo April
13,2023,bungeni Jijini Dodoma Mtaturu amesema tayari kwenye kikao cha kamati ya
ushauri ya Mkoa (RCC),ya Singida.
“Sisi wilaya ya Ikungi tuna majimbo
mawili yakiutawala lakini majimbo hayo yamepewa majina ambayo hata mtu
akiangalia haraka haraka hajui jimbo lipo wapi ,sisi hatuombi eneo jipya
tunaomba jina libadilike ,
“Tunayo Singida Mashariki na Singida
Magharibi,mfano tukipewa jina la Jimbo la Ikungi badala ya Singida Mashariki
angalu inaweza leta maana nzuri au ukiletewa jimbo la Puma au Sepuka badala ya
Singida Magharibi walau utakuwa umeweka utambulisho wa eneo husika,naamini
jambo hili sio kubwa na pacha wangu Kingu amepiga makofi ina maana anakubaliana
nami,”amesema.
Amesema dhamira ya kufanya hivyo ni
kuhakikisha kwamba wanapata utambulisho halisi ya majimbo hayo na wananchi
wajue wabunge wao wanapotaja majina ya majimbo yenye utambulisho wajue wanatoka
wilaya ya Ikungi.
MAJIBU YA SERIKALI .
Akijibu ombi hilo ,Waziri wa
Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu Jenista Mhagama amesema
wamepokea ombi hilo.
“Tumepokea ombi la mbunge Mtaturu
ameomba hapa kuangalia majina ya majimbo katika eneo analotoka,sasa ibara ya 74
kifungu kidogo cha 6 (c) na ibara ya 75 imeipa jukumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC),kuratibu,kutathimini na kujenga mipaka ya majimbo nchini,
“Kutokana hilo tunaomba muda
utakapofika Mtaturu na Kingu pelekeni mapendekezo ya majina hayo,na hasa kama
hayatakuwa na gharama ya kuyagawa na kuyapanga upya basi tutaangalia jina
litakalolingana na sifa na stahiki na matakwa ya wananchi,”amesema.
0 Comments