Mbunge wa
jimbo la Ubungo Saed Kubenea amevitaka vikundi vinavyodaiwa kuwa vya CCM
vinavyozunguka kuandikisha vitambulisho vya watu kuacha mara moja kabla
hawajachukua hatua ambazo amezitaka zisilaumiwe.
Akizungumza
jana na wanahabari, Kubenea alisema kwamba wamegundua wapo vijana ambao
wamekuwa wakilizunguka jimbo la Kinondoni na kuwalaghai wapiga kura kwa kununua
vitambulisho, kuchukua shahada pamoja na kununua vitambulisho hivyo ili
kupunguza idadi za wapiga kura kwa makusudi.
Kubenea
amesema kwamba endapo vikundi hivyo vitakaidi agizo hilo watashughulikiwa kama
wahalifu kwani kitend wanachokifanya ni kitendo cha uhalifu.
"Mnyika
alituambia kuwa wanaofanya hivyo ni vibaka kama vibaka wengine, hivyo wanapaswa
kushughulikiwa. Na sisi tunasema kwamba Tutaingiza vijana wetu mitaani ili
washughulikiwe na lolote litakalotokea wasituulize." Kubenea
Pamoja na
hayo kubenea amesema kwamba tayari wamekwishapeleka malalamiko yao katika
vyombo husika.
Kubenea kwa
sasa ndiye Kampeni Meneja wa Mgombea Ubunge wa Kinondoni, Salum Mwalimu wa
CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa kufanyika Februari 17
0 Comments