Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu amekiri kwamba hatakuja kusahau tukio
la mkazi wa Iringa aliyekwenda hospitali Nairobui alikolazwa kwa ajili ya
kumuombea ili apate kupona baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Lissu
ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini,
amedai kwamba mama huyo alimgusa sana kwa upendo aliouonyesha juu yake huku
akizingatia kwamba ametokea mbali sana huku akionekana ni mtu wa hali ya chini.
"Ukiwa
mgonjwa kisha akaja mtu kukutembelea ni faraja sana. Nawashukuru maelfu ya
watanzania na watu wote waliofika Nairobi kunijulia hali. Lakini sitakaa kuweza
kumsahau mama mmoja aliyetoka Iringa kwa ajili ya kuja kuniombea," Lissu.
Lissu ameongeza
"Aliniambia Mheshimiwa nimetokea Iringa na mpaka nimefika hapa nimetumia
siku tano. Nikamwambia mama asante niombee kisha akapiga magoti na kuniombea.
Alinigusa sana na ukimuangalia mama yule unatambua kabisa hajatokea mjini na
hata hali yake ya uchumi siyo nzuri lakini ulikuwa ni upendo wa ajabu ambao
ulinigusa sana".
Mbunge Lissu
yupo hospital ya Nairobi akipatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi na watu
wasiojulika huko mkoani Dodoma wakati akiwa ametokea kazini (bungeni) Septemba
07, 201
0 Comments