Mkuu wa Mkoa
wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, ameonya kuwa watu watakaovuruga mikutano ya
kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Singida Kaskazini, serikali
itawashughulikia kwa mujibu wa sheria.
Dk. Nchimbi
alitoa onyo hilo katika Kijiji cha Mtinko Wilaya ya Singida Vijijini alipokuwa
akitoa taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu ya tano kwenye uzinduzi wa
kampeni hizo.
Alisisitiza
kwamba ili watambue kuwa ni mtumishi aliyetumwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM),
ajitokeze mtu yeyote na kuthubutu kuvuruga ratiba ya mikutano ya kampeni.
Hata hivyo,
aliwahakikishia wananchi kuwa mikutano ya kampeni itakuwa salama pamoja na
uchaguzi huo kwani serikali imejipanga kikamilifu kudhibiti yeyote
atakayeonekana anataka kuvuruga uchaguzi huo.
“Na ole wake
na atokee mtu yeyote yule mwingine atakaeingilia katika njia hii ya uchaguzi
salama, amani na utulivu ndipo mtakapotambua kwamba nimetumwa na serikali ya
Chama Cha Mapinduzi,” alisema na kuongeza:
“Jiandaeni
vizuri na wakati wa kura mjitokeze kwa wingi kupiga kura na kumchagua mgombea
wa CCM, na siyo mwingine.”
Dk.Nchimbi
aliyataja baadhi ya mafanikio yaliyopo katika jimbo hilo ni bomba na mafuta
kutoka Horiri Uganda hadi Tanga ambalo kwa Singida Kaskazini lina sifa ya pekee
yake na litakuwa limenyanyuka kiuchumi kuliko sehemu yeyote litakapopita.
“Na hapa
Singida Kaskazini kutajengwa kambi, patajengwa kituo watakuja wataalamu na
mabingwa wa hilo bomba ambao watakaa hapa kwa zaidi ya miaka mia moja,
hawatakaa pengine bali watakuja kukaa Singida Kaskazini,”alisema.
Uchaguzi huo
unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Lazaro Nyalandu (CCM),
kujiuzulu na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
0 Comments