Mafanikio ni
hali ambayo kila mtu anapenda kuwa nayo na kuyafikia kila mara. Mafanikio
humfanya mtu afarijike, ajisikie yuko salama, afurahi na kusonge mbele kwa
ujasiri zaidi. Mafanikio humfanya mhusika kuwapenda wengine na kuwa mkarimu.
Ukikosa
mafanikio unaweza kuwa na hasira, kukata tamaa, kutawaliwa na mfadhaiko wa
akili, ulevi wa kupindukia, usinzi na kwa ujumla kuwa na tabia mbaya. Mtu
anayeshindwa kufanikiwa huwa hana ujasiri na kila mara ametawaliwa na
kushindwa, Ushirika mdogo na wenzake na sio mshauri mzuri kwa wengine
Ili
ufanikiwe unatakiwa angalau kuzingatia nguzo 7 hapa chini:
- Kupanga
- Kupenda
- Kujiamini
- Kuvumilia
- Mbadala
- Kuwajibika
- Vipaumbele
Kupanga
Wahenga
walisema usipopanga umepanga kushindwa
Walisema pia
usipokuwa na malengo kila lengo litakufikisha uendako.
Mipango ndio
inaweka majukumu ya kufanya. Mfano kama hujapanga la kufanya asubuhi waweza
kulala hata mpaka jioni bila kuona kama kuna shinda yeyote.
Kupanga
inaanzia kwa kuweka maono ya maisha yako. Unataka baada ya miaka 15/20 kuwa na
mafanikio ya namna gani katika maeneo yafuatayo
- Kiuchumi
- Kiroho
- Kielimu
- Kisiasa
- Kijamii
Kiuchumi
Panga
unatazamia kuwa na kampuni, ranchi, au ajira kwa ngazi ya mkurugenzi wa
shirika, kampuni, taasisi ya serikali wenye mshahara mkubwa kulingana na wakati
huo nk
Kiroho
Upange kuwa
maisha yako ya kiroho yatakuwaje baada ya muda huo, utakuwa mchungaji,
mwinjiisti shekhe. Au hata kiroho utakuwa umepoa au umemuishia Mungu kwa undani
zaidi nk
Kielimu
Panga kama
unategemea kuwa na digrii mbili au tatu baada ya miaka 15?
Kisiasa
Kama
unapendelea mambo ya siasa na upange kwamba baada ya miaka 15 utakuwa mbunge,
rais wa nchi nk.
Kijamii
Utakuwa na
familia ya namna gani, mke, watoto, elimu yao nk
Kupenda
Upendo
tunaouzungumzia hapa ni passion. Huu ni upendo wenye kujitoa na kuwajibika
zaidi. Kile kitu unachokifanya jitahidi sana ukipende. Kama ni kozi ya udaktari
hakikisha unakipenda na udaktari wenyewe unaupenda kiukweli. Kwa maana hii
hakikisha unachagua vizuri njia unayopita.
Penda pia na
hali ya mafanikio unayotarajia, mfano penda kuwa bilionea au msomi kwa ngazi ya
udaktari, kama ni mwanafunzi penda ile hali ya kupata alama ya “A” kwa masomo
yako nk
Usijipeleke
kwenye unesi wakati kazi za kuwahudumia wagonjwa inakupa kinaa. Ukipenda kitu
utakuwa tayari kuvumilia, kupambana na kukabiliana na changamoto zinazoambatana
na eneo husika
Kujiamini
(Kuwa mjasiri na kujiamini)
Ujasiri unakupa
mambo mengi. Kujiamini, kuchukua hatua, kuamua na kutenda hata kama wengi
wanakupinga na kukubeza
Kuvumilia
Kazi nyingi
zina changamoto tena kubwa na nyingi. hakuna kazi rahisi duniani. Usipokuwa
king;anganizi na mvumilivu utakuwa unatangatanga mara leo mikaa mara kesho
umachinga wa bango mara kesho kutwa mfanyakazi wa nyumbani mpaka uzee unakukuta
hujafanya kitu.
Uvumilivu unakusaidia wewe kuijua kazi yako na
changamoto zake na hivyo kukufanya wewe kuwa mtaalamu na guru wa eneo au sekta
husika. Hata kama imechukuwa muda mrefu huko mbeleni utatumia gharama na njia
rahisi kufikia malengo kwa sababu ya uzoefu ulionao kwenye eneo husika ambao
umesababishwa na kuvumilia.
Kumbuka pia
kuwa uvumilivu unaendana daima na kujifunza kutokana na changamoto unazokutana
nazo njiani pamoja na kuweka mipango mbadala
Mpango
mbadala (Kuwa na mpango mbadala)
Wahenga
walisema kuwa Kushindwa ni dalili kuwa mpango wako wa kwanza haufanyi kazi
hivyo weka mpango mwingine au mbadala
Pia wahenga
wengine walienda mbali zaidi na kusema
Kushindwa ni
fursa nzuri ya kufanya vizuri zaidi, safari hii kwa umakini zaidi
Aliyegundua
na kutengeneza taa alishindwa mara 10,000 na baadaye sana ndipo akagundua taa
ambayo leo inatumulikia dunia nzima kuanzia majumbani, viwanja vya ndege na
mpira pamoja na kwenye anga za juu.
Wahenga
walisema kuwa Kufanikiwa kupo kwa sababu kuna kushindwa na kushindwa kupo kwa
sababu kuna kufanikiwa
Kuwajibika
(Kuwajibika na mafanikio au kushindwa kwako)
Daima watu
wenye kufanikiwa wanawajibika kwa yale maeneo ambayo wanashindwa. Ukishindwa
jisemee ni kwa sababu sikufanya vizuri kwenye eneo X na Y nk. Usianze
kuwasingizia wenzako nk
Mfano wa
timu ya mpira
Kama wewe ni
mfungaji na ukashindwa kufunga bao la wazi, usiseme kuwa kiungo alikupa pasi
mbovu au alipaiza juu sana
Sema kuwa
nilichelewa kuuwahi mpira ndio maana nikashindwa kufunga. Siku nyingine
nitajitahidi kuwahi mpira kama huo
Kufanya kwa
vipaumbele
Utekelezaji
ndio hitimisho la mafanikio. Kama utapanga hata mipango 1,000 kama wewe
hunatabia ya kutekeleza basi mafanikio sahau kabisa.
Kuna mitego
mingi kwenye kutekeleza mambo uliyoyapanga
0 Comments