Mbunge wa
Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amefunguka na kusema kuwa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) hawawezi kulikomboa jimbo la Mbeya Mjini hata kwa mabavu
kwani anasema watu wa Mbeya hawajaribiwI hata Kikwete na Magufuli wanatambua
hilo.
Sugu amesema
hayo alipokuwa akihojiwa na MCL na kudai kuwa amesikia CCM wanasema wanataka
kukomboa jimbo la Mbeya Mjini na kudai kuwa hawataweza kwa kuwa hata wao
CHADEMA hawajalala.
"Wananchi
bado wanaridhika na sisi kwa hiyo njia pekee watakayofanya labda watumie mabavu
na kwa kutumia mabavu CCM Mbeya wanajua, Kikwete anajua, Magufuli anajua kwamba
kwa mabavu kwa Mbeya uwezo huo hawana kwa sababu watu wa Mbeya hawajaribiwi na
hilo tunalithibitisha hata kwenye Kata ya Ibighi wameleta mchezo mchezo wao
kote walikoleta kwenye kata 42 lakini walipofika Ibighi tuliwapiga 'Stop'
tukawathibiti" alisema Sugu
Sugu
aliendelea kusema kuwa "Kama kwenye uchaguzi mdogo wa Ibighi ambao
kulikuwa na resources zote za mkoa ziliwepo pale na wakashindwa kutumia mabavu
watawezaje kwenye uchaguzi mkuu ambao resources zinakuwa mbalimbali, majimbo
yanakuwa saba huko kote hao polisi wa kuwapeleka hawana kama ambavyo waliweza
kukusanya polisi wa mkoa mzima kuwapeleka kwenye Kata ya Ibighi na bado
wakashindwa" alisisitiza Sugu
0 Comments