Bwana Yesu
Asifiwe , jina langu ninaitwa Winnie, mkaazi wa wilaya ya Kisarawe mkoani
Pwani.
Kwa sasa
nimeokoka na kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yangu lakini kabla
sijaokoka nilikuwa mtumwa wa shetani kupitia uchawi.
Nimeamua
kuandika waraka wangu huu baada ya kuguswa .
Ninaona nina
wajibu mkubwa wa kuelezea siri hizi za wachawi ili niweze kuwekwa huru lakini
pia niweze kuwasaidia watu wengine waweze kuwa huru, kwani maandiko matakatifu
yanasema nanyi mtaijua kweli nayo itawaweka huru.
Nimeona si
vyema endapo nitakufa nikiwa na siri yangu hii. Mambo niliyo yapitia yamefunza
mambo mengi sana maovu yanayo tendeka katika ulimwengu huu ambayo nilikuwa
siyafahamu hapo awali.
Ninataka
ulimwengu mzima uyafahamu na hivyo kuwa huru.
Nisiwachoshe
kwa maneno mengi ila kwa ufupi tu ni hivi mwaka 2014 rafiki yangu mmoja
alinipeleka kwa mganga wa kienyeji ili anisaidie niweze kupata mume wa kuniona.
Nilifikia
uamuzi huu baada ya mwanaume alie kuwa anataka kunioa kufariki ghafla kwa ajali
ya gari huku akiniacha na kichanga cha minane tumboni.
Tukio hilo
lilini huzunisha sana kwa sababu mwaka huo wa 2014 nilikuwa nimetimiza umri wa
miaka 40 nikiwa bado naishi nyumbani kwa wazazi wangu huku nikiwa na watoto
wawili huku kila mmoja akiwa na baba ake.
Nilimfuata
dada mmoja jirani yangu ambae alikuwaga ananisaidia hela na chakula kila
nilipokuwa naenda kumuomba
Nilipo
mfuata kuomba ushauri nifanye nini, nilimuelezea historia yangu yote kuanzia
mume alietaka kuniona wakati bado nipo msichana kisha akaingia mitini kabla
ndoa haijafungwa, mwanaume nilie zaa nae mtoto wa kwanza, wapili hadi huyu ambae
amefariki na kuniacha na kichanga cha miezi minane.
Dada huyu
akaniambia atasaidia kunihudumia hadi nitakapo nijifungua na nikisha jifungua
atanipeleka kwa mganga ambae atanisaidia.
Kweli
alifanya kama alivyo niahidi. Bahati mbaya mtoto hakuwa riziki. Alizaliwa akiwa
amefariki tayari.
NAPELEKWA
KWA MGANGA
Tulipofika
kwa mganga akanitazama na kuniambia kuwa nimefungwa kichawi.
Mganga
akaniambia kuwa nyota yangu iliibwa kichawi muda mrefu kwa ajili ya kwenda
kutumikishwa kichawi.
Mganga
akaniambia hakuna haja yoyote ile ya kuirudisha nyota hiyo kwa sababu
imeshakufa huko ilipo na haiwezi kunisaidia kitu chochote hata kama itarudishwa
kwa sababu imetumikishwa .
Akaniambia
ilikuwa niolewe tangu nikiwa na miaka 20,lakini “ndoa” yangu ilibatilishwa
kichawi kwa kutumia bundi na bahati yangu ya kuolewa akapewa mwanamke mwingine.
Na kweli kwa
mujibu wa kumbukumbu zangu, nikiwa nina umri huo kuna mwanaume mmoja alitaka
kunioa lakini badae ndoa ikapeperuka hata sijui kitu gani kilitokea.
Mganga
akaniambia kwa kuwa bahati yangu ya ndoa iliibwa kwa kutumia bundi basi na mimi
itabidi niibe bahati ya mtu mwingine kwa kutumia bundi.
Sikuwa na
jinsi Zaidi ya kukubaliana na mganga pamoja na kwamba sikujua lingewezekanaje
hilo..
NAAMBIWA
NIKACHUME MTI WA PILIPILI NIKIWA KWENYE SIKU ZANGU.
Mganga
akaniambia nirudi nyumbani, halafu siku nitakapo ziona siku zangu basi niende
kwenye mti wa pilipili nichume pilipili halafu niutazame vizuri huo mti kisha
nimjulishe nimeona nini.
NACHUMA MTI
WA PILIPILI NIKIWA KWENYE SIKU ZANGU
Siku
nilipoziona siku zangu nikaenda kuchuma pilipili. Niliona kitu cha ajabu sana.
Kitu ambacho sikuwahi kukiona tangu nizaliwe.Ule mti wa pilipili ulikauka
ghafla. Niliogopa sana nikampigia mganga. Mganga akaniambia niuchume huo mti halafu
kesho niende nikamuone.
NAPELEKA KWA
MGANGA MTI WA PILIPILI ULIO KAUSHWA NA HEDHI
Kesho yake
nikadamkia kwa mganga na mti wa pilipili ulio kauka. Mganga akauchukua huo mti
na kuusaga pamoja na dawa zake nyingine anazo zijua yeye mwenyewe. Baadae akanichanja
akanipaka mafuta ambayo sikujua ni mafuta ya nini. Akanipa dawa za kuoga, na
kunywa pamoja na hirizi.
Halafu
akanipa dawa ya kuchoma usiku.
MGANGA
ANANIELEKEZA NAMNA YA KUWAITA BUNDI NA KUWASILIANA NA BUNDI KWA ISHARA.
Mganga
akaniambia haya mafusho ninayo kupa ni uchawi mkubwa sana.
Zingatia
masharti yote nitakayo kupa vinginevyo utapata madhara makubwa sana.
Akaniambia
hilo ni fusho maalumu la kuwaita bundi. Kwa kutumia fusho hilo utakuwa unawaita
bundi na kwa kuwatumia bundi hao utaweza kujua ni katika nyumba gani kuna
mwanamke mwenye bahati ya kuolewa.
Kupitia
bundi utaweza kujifunza vitu vingi sana ambavyo ulikuwa hauvijui.
Mbali na
kujua mwanamke gani ana bahati ya kuolewa, unaweza kujua kwenye nyumba gani
kuna watu wana nyota nzuri nakadhalika.
Mganga
akaniambia nitakufundisha namna ya kutafsiri ishara mbalimbali za milio ya
bundi.
i. Bundi
akilia mara moja, anatoa ishara kuwa katika nyumba hiyo kutatokea msiba hivi
karibuni. Na hapo itategemea amelia saa ngapi. Kama akilia kati ya saa sita na
saa saba usiku basi anakuwa anatoa ishara ya kutokea kwa msiba na kama kama
atalia kati ya saa 4 na saa 5 usiku anakuwa anatoa ishara na kuwaonya wenye mji
juu ya ujio wa wachawi katika mji huo usiku huo.
Hii ni kwa
sababu bundi anaweza kuona mambo ya sirini, mambo aliyo fichwa mwanadamu na
mambo yatakayo tokea siku za mbeleni.
ii. Bundi
akilia mara mbili maana yake ni kwamba wewe ulie isikia sauti hii utapata
mafanikio makubwa sana katika kitu unacho taka kukianzisha hivi karibuni, na
ili ufanikiwe katika kitu au jambo hilo ni lazima ukifanye haraka iwezekanavyo.
iii. Bundi
akilia mara tatu basi anatoa ishara kwamba katika nyumba iliyopo karibu na mti
ambao bundi huyo alitua wakati analia, kuna mwanamke ataolewa na ndoa yake
itadumu kwa muda mrefu.
iv. Bundi
akilia mara nne anakuwa anatoa ishara kwamba wakaazi wa nyumba au mtaa huo
watapata usumbufu mkubwa katika siku za karibuni.
v. Bundi
akilia mara tano anatoa ishara kwamba wewe ulie sikia sauti hiyo utapata safari
nzuri hivi karibuni.
vi. Bundi
akilia mara sita anatoa ishara kwamba, kuna wageni wapo njiani wanakuja
kuwatembelea.
vii. Bundi
akilia mara saba anatoa ishara kwamba kuna mtu au watu katika nyumba hiyo
watapatwa na matatizo ya msongo wa mawazo.
viii. Bundi
akilia mara nane, anakuwa anatoa ishara kwamba katika nyumba hiyo utatokea
msiba wa ghafla.
ix. Bundi
akilia mara tisa anatoa ishara ya bahati njema katika nyumba hiyo.
Sasa basi,
wachawi huwa wanakuwa makini sana kusikia sauti za bundi pindi wanapolia. .
Baada ya
hapo mganga akaniambia natakiwa kwenda kumwaga mafusho hayo kidogo kwenye mti
wowote mkubwa ulio jirani na nyumba ambayo nimeikusudia na kuchukua jani la huo
mti kwenda nalo hadi chumbani kwangu kisha kulichoma kwenye chetezo pamoja na
hayo mafusho huku nikitamka maneno maalumu ya kuwaita bundi waje kwenye huo mti
ili waweze kujua ni mwanamke gani anakaribia kuolewa ndani ya nyumba hiyo.
Usiku wa
siku hiyo nikafanya kama nilivyo elekezwa. Nikaenda kuchuma jani la huo mti na
kuwamga fusho kidogo kwenye mti kisha ilipofika saa tatu za usiku nikaanza
kuchoma ilo fusho pamoja na jani la huo mti.
Ilipofika
saa sita usiku kweli bundi wakaja na muda si mrefu wakaanza kulia. Nikasikia
kwa makini sana.
Bundi akalia
mara tatu . Alilia kutoka kwenye mti uleule ulio jirani na nyumba ya shangazi
yangu. Nilichagua mti ulio jirani na nyumba ya shangazi yangu kwa sababu
shangazi yangu alikuwa na watoto wengi wa kike na nyumba yake ilikuwa na wageni
na wapangaji wengi wanawake.
Mganga
aliniambia bundi wakisha nyamaza tu nimjulishe haraka sana.
Kama alivyo
nielekeza mganga nikamjulisha.
Nilipo
mjulisha akaniambia sawa, nilale halafu kesho asubuhi nihakikishe naenda kwa
shangazi yangu au naongea na mtu yoyote anaeishi nyumbani kwa shangazi yangu.
Nitakapo kuwa
hapo kwa shangazi yangu nisikie kama watazungumza chochote kuhusu bundi na kama
wasipo zungumza basi nijifanye kuanzisha mazungumzo kuhusu bundi, nijifanye na
mimi jana bundi walitua nyumbani kwetu na kwamba ninaogopa sana.
Na watakacho
nijibu basi nimjulishe mganga.
Kweli
nikaenda hadi kwa shangazi na bahati nzuri nikamkuta binamu yangu ambae ndio
nilibatilisha ndoa yake kichawi.
Binamu
hakuwa na dalili zozote za kupiga story kuhusu bundi hivyo nikaanzisha story za
bundi kwamba jana bundi walilia sana batini kwangu na kwamba nilishindwa
kulala.
Binamu
akaniambia hata kwao ilikuwa hivyo hivyo na sio kulia tu bali kuna wakati bundi
waliingia hadi ndani wakatua na kuondoka.
Tukaongea
kwa muda kidogo kisha baada ya hapo nikampigia mganga na kumueleza kila kitu.
Mganga
akaniambia vizuri sana, mambo yako yatakuwa mazuri sana.
Niseme kitu
kimoja, wachawi kwa kumtumia bundi, wakishajua kwenye nyumba Fulani kuna mtu
ana nyota ya kuolewa hivi karibuni au kuna watu wenye nyota kali wamelala
kwenye nyumba hiyo huwa wanawatuma bundi kwenda kuiba nyota hizo.
Hivyo basi
siku ukisikia bundi wamelia mara tatu karibu na nyumba yenu halafu baadae
wakaingia ndani basi jua bahati ya kuolewa ya mtu imeibiwa na kama kuna watu
wenye nyota kali walikuwa ndani ya nyumba hiyo basi na nyota zao zinakuwa
zimechukuliwa pia.
Hivyo ndivyo
alivyo niambia Dokta na akaniambia ikitokea nimeenda kwenye mji wa ugenini
halafu jambo hilo likatokea, basi nihakikishe huyo bundi atakae ingia ndani
anauliwa au anakamatwa kabla hajapaa,jambo ambalo hata hivyo ni gumu sana kwa
sababu bundi wanapo ingia ndani huwezi kuwasikia kwani huwa wanapaa bila kupiga
kelele wala kutoa sauti.
Dokta
akaniambia huu ni uchawi unao tumika sana na hautumiki kwenye masuala ya
mapenzi tu bali biashara pia.
Akaniambia
wafanya biashara wengi wametajirika na wanaendelea kutajirika kwa kutumia
uchawi huu wa kuiba nyota za watu kwa kuwatumia bundi.
Na hii ndio
sababu bundi anatukuzwa sana miongoni mwa wafanya biashara.
Mganga
akaniambia ili nyota isichukuliwe na bundi kwa staili hiyo natakiwa niwe na
kinga maalumu ya kuwazuia bundi kuchukua nyota.
Akasema
kinga hii ni tofauti na kinga zingine zote na kwamba hata kama una kinga
nyingine yoyote ile lazima kinga hii uwe nayo pia.
Akaniambia
kwa kuwa nimeingia kwenye mtandao huu inabidi hiyo kinga niwe nayo.
Siku ya
kutengeneza kinga hii,mganga alichukua paka mweusi, akauliwa kisha akatobolewa
macho halafu kwenye macho yake zikawekwa mbegu za mti wa mnyonyo kila jicho.
Paka huyo
akafungwa kwenye kitambaa cheupe mfano wa maiti akawekwa kwenye mfuko nikapewa
kwenda nae na kumzika vichakani kwenye eneo ambalo nitaliweka alama… Nikawa
namwagilizia maji kila siku hadi mti ulipo chipuka na kukua.. Mti ulipo kua
mganga akaniambia nitoe mbegu, nikafanya kama alivyo nielekeza . Mganga akaniambia
nichukue mbegu saba kisha nimpelekee.
Nilipo
mpelekea mbegu hizo mganga, akazichukua akachanganya na dawa zake anazo zijua
mwenyewe akachukua popo,akamkata kucha akiwa hai na kumuacha, akaziasaga na
muzichoma kisha kunichanja na kunipaka.
BAADA YA
BUNDI KULIA NA KUTUA KWENYE NYUMBA YA SHANGAZI YANGU
Sikuwa najua
kama binamu yangu mtoto wa shangazi yangu alikuwa na mpango wa kuolewa kwa
sababu ni jambo lililofanywa siri.
Lakini siku
chache baada ya bundi kutua kwenye nyumba ya shangazi yangu nikaanza kusikia
habari za kuharibika kwa mipango ya ndoa ya binamu yangu.
Binamu yangu
alitaka kujaribu kujiua baada ya mume mtarajiwa kugombana nae na kuingia mitini
na kisha kuhamishia uchumba kwa mwanamke mwingine.
Wakati huo
huo,mimi nikapata mwanaume mwenye pesa ambae alinichumbia na kunioa tena kwa
harusi kubwa.
Ni hivi
bahati ya ndoa ya mtu inayo ibwa kwa kutumia bundi, sio lazima wewe uolewe na
aliekuwa anataka kumuoa mwanamke uliye iba bahati yake.HAPANA. Ni hivi inaweza
kutokea mwanaume huyo labda akafukuzwa kazi ghafla au akafilisika na mipango
yake kuvurugika.
Nyota ya
mwanaume huyo inaibwa anapewa mwanaume mwingine ambae atakuja kukuoa wewe.
NAAMUA
KUACHANA NA USHIRIKINA NA KUMRUDIA MUNGU.
Niliishi na
mwanaume huyo toka 2014 hadi 2016 katikati.. Siku moja nilipokea taarifa za
msiba wa rafiki yangu ambae ndio aliniunganisha na huyo mganga.
Huyu dada
alikuwa anaishi maisha ya kidini lakini kumbe alikuwa anafanya ushirikina sana.
Kuhusu kifo
chake, sijui kama kilitokana na ushirikina ama ni mipango ya mungu lakini
nilipo ona mwili wake niliogopa sana.
Niliwaza
nakuwazua, nilitafakari nakutafakari. Nikajiuliza moyoni kumbe na mimi pamoja
na mali na pesa hizi nilizo zipata kwa njia ya ushirikina ipo siku nitakuwa
kama huyu ?
Kumbe mimi
sio kitu kabisa katika dunia hii ? Kumbe binadamu ni mchanga.
Kumbe
binadamu ananuka na kutoa harufu ? Kumbe ipo siku ndugu zangu wataogopa kulala
na mimi ?
Nilitakafakari
sana .. Nilikumbuka mambo mengi ya utotoni. Jinsi nilivyo lelewa na wazazi
wangu.
Nililelewa
kufuata maadili ya Mungu na kuwa mvumilivu na mstahimilivu kwa namna yoyote
ile.
MAHUBIRI YA
MCHUNGAJI WAKATI WA MAZISHI YANILIZA
Nikiwa
katika hali ya majuto na uchungu mkubwa Mchungaji alianza kuhubiri neno la
Mungu.
Alihubiri
mambo mengi sana lakini kikubwa aliwasisitizia waombolezaji kumkumbuka Mungu
wakati wa uhai wao na kwamba hapa duniani tunapita tu.
Mchungaji
waliwaasa waumini wasiwe na tamaa na mali za duniani hapa kwani tutaziacha
hapahapa duniani.
Mchungaji
akawakumbusha waumini kwa kuwasomea neno la Mungu kutoka katika kitabu cha
MATHAYO 16 : 26 ambalo linasema
“Kwa maana
mtu atapata faida gani akiupata ulimwengu wote lakini aipoteze nafsi yake?au
mtu atatoa nini ili aipate nafsi yake?”
Hapa
Mchungaji akawa kama ananiongelea mimi kabisa.
Baadae akasema
najua kuna watu wanakata tamaa ya kufanikiwa katika maisha kwa sababu
wamehangaika muda mrefu bila mafanikio.
Shetani
anazitumikisha nafsi zao kwa faida yake na watu wake. Wametupiwa nuksi na
mikosi na wachawi.
Mungu
anasema katika kitabu cha YOELI 2 Sura ya 25 Nami nitawarudishia hiyo miaka
iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa
nililotuma kati yenu…
Baadae
Mchungaji akasema kama kuna watu wapo tayari kuokoka basi na wanyooshe mikono
yao nami nitawaongoza sara ya toba.
Nilidhani ni
mimi tu nitakae nyoosha mkono wangu lakini nilishangaa kuona na watu wengine
wengi tu wakinyoosha mikono yao.
Hata yule
binamu yangu ambae niliiba nyota yake kichawi nae alinyoosha mkono wake. Wote
tuliombewa na baadae tukaanza mafundisho kanisani na hadi muda huu ninaondika
waraka huu bado tunaendelea kumtumikia Mungu.
KUHUSU MUME
WANGU : Mume wangu alinikimbia baada ya kuona nimeokoka jambo ambalo
nililishukuru pia kwa sababu hakuwa haki wala staili yangu.
MAISHA YETU
YA MAHUSIANO KWA SASA.
Kwa sasa
mimi nina mchumba na yule binamu yangu ameshaolewa tayari.
KUHUSU
MGANGA ALIYE NIINGIZA KWENYE SUALA LA KUIBA NYOTA ZA WATU KWA KUMTUMIA BUNDI.
Mganga huyu
anajulikana Zaidi kama mungu wa kabili na namba zake za simu ni 0744 -000 473.
NIMEWEKA JINA
LAKE NA NAMBA ZAKE ZA SIMU ILI WATU WAJUE KWAMBA HUYU NI MCHAWI NA WAKALA WA
WACHAWI NASHETANI NA WAEPUKANE NAE KWA SABABU ATAWAINGIZA KWENYE MAMBO YA
UTUMWA WA ULOZI NA UCHAWI KAMA ALIVYO FANYA KWANGU.
1 Comments
Karibu Tiba asili na Dokta, Mdirokupata tiba mbalimbali kupitia visomo na dawa mbalimbali..
ReplyDeletePIGA SIMU No, 0742162843...
Kwa wale wasumbuliwao na magonjwa sugu na matatizo kama
Kusafisha nyota, biashara, kumvuta mpenzi, KUTENGENEZA MALI KWA NDAGU au KUTENGENEZA MALI KWA MAJINI, kulinda mali, kulinda familia, Utulivu katika ndoa, kuitambua nyota yako, Kwa wale wasumbuliwao na majini(mapepo) na mengine mengi kumbuka husitume sms tafadhali piga simu kuhepuka matapeli.
KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA KWA MASWALA YA KUPATA PESA ZA NDAGU AU MAJINI......
piga namba +255742162843
(KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI...
Naitwa Dokta Mdiro, piga simu 0742162843 kwa maelezo zaidi...
UTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
(kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
1. uwe una umri wa miaka 18+
2. uwe tayari kupokea masharti yote
3.uwe na uwezo wa kutunza siri
4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.