Ushindi wa
goli 1-0 ilioupata timu ya Singida United dhidi ya Lipuli unaifanya timu hiyo
ya mkoani Singida kufikisha pointi 17 sawa na Yanga pamoja na Mtibwa Sugar.
Licha ya
kufungana pointi na timu hilo (Yanga na Mtibwa) Singida United ipo nafasi ya
tano kutokana na wastani wa magoli. Tayari timu hiyo imeshacheza mechi 10 za
VPL sawa na Lipuli huku vilabu vingine vikiwa vinataraji kucheza michezo ya
mzunguko wa 10 kesho Jumamosi na keshokutwa Jumapili.
Singida
United imepata ushindi wake wa kwanza kwenye uwanj wa nyumbani (Namfua) tangu
imepanda kucheza ligi kuu msimu huu, awali timu hiyo ilikuwa ikiutumia uwanja
wa Jamhuri Dodoma wakiwa wamepisha ukarabati wa uwanja wa Namfua. Mechi yao ya
kwanza kucheza uwanja huo msimu huu ilikuwa dhidi ya Yanga ambapo ilimalizika
bila timu hizo kufungana.
Kikosi cha
Hans van Pluijm kimepata ushindi wa kwanza baada ya kutoka sare katika mechi
tano mfulizo zilizopita. Ushindi huo ni wa nne katika mechi 10 ambazo tayari
wamecheza. Singida imepoteza mechi moja tu msimu huu ambapo ilifungwa 2-1 na
Mwadui kwenye mechi yao ya kwanza.
0 Comments