Serikali ya
Afrika Kusini imesema Rais Robert Mugabe amekutana na wajumbe kutoka nchi za
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika( Sadc) katika juhudi za kujaribu kutatua
mzozo wa kisiasa nchini humo.
Alisafiri
hadi kwenye ikulu kutoka makao yake ya kibinafsi ambako amekuwa akizuiliwa na
jeshi.
Wanajeshi
waliingilia kati na kutangaza kudhibiti serikali Jumatano katika kinachoonekana
kuwa juhudi za kumzuia mke wa Mugabe, Grace, asitwae madaraka.
Duru
zinadokeza kwamba Bw Mugabe anataka kusalia madarakani hadi wakati wa kufanyika
kwa uchaguzi mwaka ujao.
Lakini
mpinzani wake wa muda mrefu Morgan Tsvangirai amemtaka ajiuzulu mara moja kwa
maslahi ya taifa.
Makamu wake
wa zamani Joice Mujuru pia ametaka kuwe na serikali ya mpito na pia uchaguzi
huru na wa kuaminika.
Mzozo wa
Zimbabwe pia unajadiliwa katika mkutano wa jumuiya ya nchi za kusini mwa
Afrika, SADC, nchini Botswana.
0 Comments