Waumini wa
dini ya Kiislam wa Msikiti wa Noor uliopo katika Kijiji cha Mkange, Miono,
Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani ,wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada wa zulia la kuswalia na fedha
taslim Shilingi milioni Mbili.
Zulia pamoja
na fedha hizo zimekabidhiwa na Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka Mkeremy kwa
niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Imamu wa Msikiti huo Alhaji Sheikh
Khamis Nassor wa Msikiti Noor uliopo katika kijiji cha Mkange, Wilaya ya
Chalinze mkoa wa Pwani.
Mara baada
ya kukabidhi Zulia na fedha hizo, Kanal Mkeremy kwa niaba ya Rais Magufuli
amewataka waumini wa Msikiti huo kutumia msaada huo kwa lengo lililokusudiwa.
Akiungumza
mara baada ya kukabidhiwa Msaada huo, Sheikh Nassor amesema kwa niaba ya
waumini wa Msikiti huo wanamshukuru Mhe. Rais kwa kuitikia ombil lao la kupata
zulia, na kwamba kwa kutimiza ahadi yake hiyo Mhe. Rais amedhihirisha kuwa yeye
ni mtu wa watu asiyebagua dini wala kabila katika kusaidia jamii ya kitanzania.
Sheikh
Nassor amesema waumini wa msikiti huo wanamuombea na wataendelea kumuombea
Mheshimiwa Rais na kuwataka watanzania wote nchinikuungana nao kumuombea Rais
bila kujali itikadi za kisiasa ama imani za kidini kwani anayoyafanya Rais kwa
wananchi wa Tanzania ni kwa manufaa ya wananchi wote.
0 Comments