Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa
aliyekuwa mwanachama wao, Lawrence Masha hakuwa na msaada wowote ndani ya chama
hicho.
Amesema kuwa
kuondoka kwa Masha katika Chama hicho hakijatikisika chochote bali kinazidi
kuimariki na kupokea wanachama wengi wapya, hivyo kuondoka kwa mtu asiyekuwa na
msaada ndani ya chama hicho si tatizo.
“Alikuwa
hatusaidii chochote ndani ya maji, kwani ulishawahi kumsikia amefanya chochote
akiwa chadema? acha amfuate babu yake, acha aondoke zake, sisi hatujapoteza
chochote, hata alipokuwa waziri alifanya nini, acha aende kwenye biashara zake
Uingereza maana tunasikia anawekeza kule,”amesema Mbowe
\Masha
alitangaza uamuzi wa kuondoka Chadema kupitia taarifa yake iliyosambazwa
kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya kuamua kuachana na Chadema
huku akisema chama hicho kinasafari ndefu ya kuweza kutwaa dola.
0 Comments