Jeshi la Zimbabwe limesoma taarifa kwenye kituo cha runinga
cha serikali ZBC, likisema kuwa linachukua hatua ya kuwalenga wahalifu.
Hata hivyo limesema kuwa hayo sio mapinduzi ya kijeshi na
Rais Mugabe yuko salama.
Milio mikubwa ya risasi ilisikika katika maeneo ya kaskazini
mwa mji mkuu Harare mapema leo.
Taarifa hiyo ya jeshi ilikuja saa kadhaa baada ya jeshi
kudhibiti kituo cha ZBC.
Mwanamume mmoja ambaye alikuwa amevaa sare za jeshi alisema
kuwa jeshi linataka kukabiliana na watu ambao wanatenda uhalifu unaoleta
madhara ya kijamii na kiuchumi nchini Zimbabwe.
"Wakati tutakapomalzia wajibu wetu, tunatarajia kuwa
hali itadudi kuwa sawa."
Taarifa hiyo ilisema kuwa Mugabe 93, na familia yake wako
salama.
Haijulikani
ni nani anaongoza hatua hiyo ya kijeshi.
Magari ya
wanajeshi waliojihami kwa silaha yameonekana maeneo ya mjini Harare.
Hali hiyo ya
wasi wasi wa lolote kuweza kutokea, imeanza hapo jana jioni, ambapo wanajeshi
wakiwa na silaha walionekana wakijipanga katika maeneo kadhaa pamoja na
kuzingira ofisi za shirika la utangazaji la Zimbabwe ZBC.
0 Comments