Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefikia uamuzi wa kumuachia Dk Louis
Shika ‘bilionea wa nyumba za Lugumi’ baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya
kujidhamini yeye mwenyewe baada ya kukosa mtu yeyote aliyejitokeza kwenda
kutaka kumwekea dhamana.
Kamanda wa
kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema “uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea
lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyefika kutaka kumwekea dhamana, yaani
anaishi kama mtu wa nyikani.”
Mambosasa
ameongeza, “nimeagiza watendaji wangu wamwachie kwa dhamana yaani ajidhamini
yeye mwenyewe na awe anakuja kuripoti,”
Dk Shika
tangu siku hiyo amekuwa gumzo sehemu mbalimbali kutokana na kile alichokifanya
siku ya mnada alipokuwa akipandisha bei dhidi ya washindani wake na moja ya
kauli zake zinaendelea kutumika hadi sasa ni ‘Mia 900 itapendeza.’
0 Comments