Follow us

AZIZKI: SINA MATARAJIO YA KUONDOKA YANGA KWA SASA

Tangazo

 

AZIZKI: SINA MATARAJIO YA KUONDOKA YANGA KWA SASA

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI baada ya timu yake kutolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Mamelodi Sundowns kwa mikwaju ya penalti hatua ya robo fainali, ameandika katika ukurasa wake wa Instagram ujumbe wa kuwashukuru mashabiki kwa kuwa nao pamoja kwenye safari ya michuano hiyo msimu huu 2023/2024.

KI ameandika; “Tumeonyesha sisi ni timu kubwa na tuna malengo, licha yachangamoto zote tutafika tunapotaka kwenda, kwani sisi ni timu kubwa,haikuwezekana msimu huu lakini tutakuwa bora zaidi wakati mwingine.”

“Kipekee kabisa niwashukuru wote waliokuwa na sisi kwenye safari hiihasa Rais wa nchi, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kujitolea kwake kwetu ilituweze kuwa bora zaidi katika mechi zetu, tulienda Afrika Kusini kama washindina tutarudi Tanzania washindi pia, ila tumejifunza mengi ya kutufanya kuwa borazaidi wakati mwingie.”

Katika ujumbe huo KI pia amemjibu shabiki aliyeandika kuhusu yeyekuondoka klabuni hapo msimu ujao kutokana na kufanya vizuri kwenye mashindanona klabu nyingi kutaka huduma yake.

Ameandika; “Huna baya mwamba sana, najua msimu ujao utaondoka maananaona Mamelodi wanataka kukusajili, najua utaondoka.”

KI amejibu; “Sina matarajio ya kuondoka Yanga kwa sasa kwanisijafanikisha malengo yaliyonileta hapa, bado klabu hii ninayoipenda kwa moyowangu wote inanidai, hata pesa haitaweza kujaza upendo nilionao kwa klabu hii,lala kwa amani shabiki bado sijamaliza dhamira yangu.”

Ikumbukwe KI amebakiza miezi minne kumaliza mkataba wake na Yanga ambaoalisaini msimu wa 2022\2023.

Post a Comment

0 Comments