MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amebainisha kuwa mpango mkubwa kwenye mechi za kimataifa ni kupata ushindi wapo tayari kutokana na maandalizi ambayo wanayafanya kwenye uwanja wa mazoezi.
Mchezo wao uliopita kwenye ligi Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC huku wachezaji wake wawili wakipata maumivu ikiwa ni Pacome Zouzoa na Yao Atohoula ambapo kwa sasa wanaendelea vizuri baada ya kupewa matibabu.
“Mechi za kimataifa zina utofauti wake hilo lipo wazi na tumekuwa tukifanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kupata matokeo chanya kwenye mechi zetu ambazo tutacheza na tunatambua kamba wapinzani wetu wanahitaji ushindi kama ambao sisi tunautafuta.


0 Comments