RASMI…..SIMBA WAKUBALI YAISHE KWA INONGA….WATAJA BEI WANAYOTAKA KUMUUZA…
UONGOZI wa
Simba umeweka wazi kuwa endapo itakuja ofa kubwa ya mabilioni ya fedha
watatengeza msimamo na kuzungumza na klabu ambayo inahitaji huduma ya beki wao
wa kimataifa, Enock Inonga Baka.
Hivi
karibuni kuna taarifa kuwa kocha wa
zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi anayekinoa kikosi cha AS FAR Rabat ya Morocco
anahitaji huduma ya beki kisiki wa
Simba, kwa lengo la kukuiongezea nguvu
kikosi chake kinachoshiriki Ligi Kuu ya nchini hiyo maarufu kama Botola Legue.
Pia inadaiwa
Al Ahly ya Misri nao wameonyesha nia
kumtaka beki huyo mwenye thamani ya Dola laki tano ambayo sawa na
shilingi bilioni 1.2 ambaye amebakisha mkataba wa mwaka mmoja ndani ya timu
hiyo.
Meneja wa
Idara ya Habari na Mawasiliano Simba,
Ahmed Ally amesema hawajapokea taarifa kutoka klabu yoyote ambayo
inahitaji mchezaji wao huo na kwa sasa hawako tayari kumuuza.
Amesema
licha ya kuweka tahadhari juu ya mchezaji huyo aliyekuwa kwenye majukumu ya
timu ya Taifa lake DR Congo kutouzwa lakini watabadilisha msimamo wao huo
endapo kutatokea timu imeenda na ofa kubwa.
“Inonga yupo
kwenye majukumu nchini Ivory Coast na
timu ya Taifa katika michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika wametinga hatua
ya robo fainali, hakuna ofa iliyofika
kwenye meza yetu licha ya sisi kuona hizi taarifa za kutajwa FAR Rabat na Al
Ahly katika mitandao.
Ninachosema
watu waogope matapeli. Kama kuna ofa kubwa tunazungumzia mabillion yakija
mezani kwetu hilo ni suala lingine na litazungumzika,” amesema Ahmed.
Kuhusu
kiungo wao Clatous Chama kusamehewa na kujiunga kambini, Ahmed amesema taarifa
juu ya nyota huyo wataiweka wazi kwa sababu alisimamishwa kwa maslahi ya klabu
pamoja na mchezaji husika.
“Kuhusu
taarifa za Chama tutaweka wazi ni
mchezaji wetu, kama amesamehewa au bado anaendelea na adhabu yake ya utovu wa
nidhamu hilo tutaliweka wazi,” amesema Ahmed.
Licha ya
Simba kutoweka wazi juu ya kiungo huyo lakini inaelezwa kiungo huyo amesamehewa
na kupewa onyo kali na amerejea kikosini kujiunga na wenzake kujiandaa na
michezo iliyopo mbele yao ikiwemo ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mashujaa
FC, Tabora United na Azam FC mechi za
viporo.
0 Comments