SIMBA mapema tu ilikamilisha lengo la
kuandika rekodi mpya ikiwapoteza watani zao wa jadi Yanga katika tamasha lao.
Simba ilikuwa ni Agosti 6 2023
iliandika rekodi hiyo kwenye tamasha la Simba Day ikiwa ni tamasha
lililokusanya mashabiki wengi nje na ndani ya uwanja.
Kutokana na jambo hilo Simba inayonolewa
na Kocha Muu, Roberto Oliveira ilikamilisha mpango wa kuandika rekodi mpya
baada ya majira ya saa mbili asubuhi mashabiki kuanza kuingia uwanjani tayari
kwa kushuhudia sherehe za Simba Day.
Hapo awali uongozi wa Simba
ulitangaza kufungua mageti saa mbili asubuhi jambo ambalo liliwafanya mashabiki
wa timu hiyo kufika mapema na kuanza kuingia uwanjani.
Mashabiki wengi waliotupia uzi wenye
rangi nyeupe na nyekundu walikuwa uwanjani kushuhudia namna shughuli hiyo
itakavyokuwa.
Lakini hiyo haitoshi rekodi nyingine
ni ile ya mashabiki wa Simba hadi kufikia saa 5 asubuhi kujaza nusu ya uwanja
wakisubiri shughuli yao ya Simba Day.
Mwisho kabisa mpaka tamasha
linakamilika uwanja ulikusanya full haouse kutokana na hamasa kubwa
iliyofanyika kila kona.
Mchezo uliokuwa unasubirwa kwa shauku
kubwa ni ule wa kimataifa wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Power Dynamo na
baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-0 Power Dynamo.
0 Comments