Zaidi ya nyumba 19 zimeteketea kwa moto katika kitongoji cha Shaurimoyo kijiji cha Nyamwage Kata ya Mbwara ,Rufiji ,Pwani mara baada ya mwananchi mmoja akiwa anasafisha eneo lake kwa moto ndipo ulimshinda na kuteketeza nyumba zipatazo 19 za wananchi pamoja na mali na thamani zilizopo ndani ya nyumba hizo .
Aidha
hakuna majeruhi yoyote katika ajali hiyo wala kifo.
Kufuatia janga hilo ,Mkuu wa mkoa wa
Pwani Aboubakari Kunenge pamoja na wajumbe wa kamati ya usalama ya wilaya ya
Rufiji wamefika kwenye tukio la moto lililotokea usiku wa kuamkia agost 30
mwaka huu, ili kuona athari iliyotokea na jitihada ambazo uongozi wa wilaya
wamezichukua kuhakikisha wananchi wanakuwa salama.
Kunenge alitoa pole kwa serikali ya
wilaya pamoja na wananchi waliokutwa na madhira hayo na kuwapongeza wakazi wa
maeneo ya karibu kuweza kuwapatia hifadhi wananchi wenzao waliokutwa na ajali
hiyo .
Aliuagiza uongozi wa wilaya hiyo kufanya haraka kujua
tathmini ya athari iliyopatikana ili kuweza kuwasaidia waliopata ajali hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya
Rufiji Meja Edward Gowele ,alieleza kama wilaya hatua walizochukua baada ya
kutokea tukio hilo .
Alitoa rai kwa wakazi wa wilaya hiyo
kuwa makini wakati wanachoma moto kwani kwa sasa ni kipindi cha upepo mkali.
Wananchi wa eneo hilo nao wameeleza
tukio jinsi lilivyowaathiri hivyo kuomba serikali kuweza kuwasaidia kwa haraka
maana hawana mahala pakuishi.
0 Comments