
Waandalizi wa michuano ya kombe la mataifa ya Akrika Misri
waliorodheshwa katika kundi zuri ambalo huenda likawapendelea lakini mabingwa
wengine kama vile Morroco , Ivory Coast na Afrika kusini waliwekwa pamoja
katika kundi gumu.
AFCON 2019: Ratiba na Matokeo ya mechi
Wafahamu wachezaji watakaoshiriki kombe la Afcon
Je unawafahamu wachezaji 'hatari' wa timu za Afrika
mashariki Afcon?
Hatahahivyo kuna mambo kumi usioyafahamu kuhusu kombe la
Afcon 2019.
1 - Misri itaandaa kwa mara ya tano kombe la Afcon. Walikuwa
wenyeji wa kombe hilo 1959, 1974, 1986 na 2006, wakiibuka washindi katika
michuano minne na kumaliza katika nafasi ya tatu katika mchuano wa mwisho.
2 - Ni mataifa matatu pekee, wenyeji Misri , Sudan na
Ethiopia walioshiriki katika mchuano wa kwanza mnamo mwezi Februari 1957 na
kulikuwa hakuna michunao ya kufuzu.
3 - 2019 Utakuwa mchuano wa kwanaza utakaoshirikisha mechi
24 , baada ya Caf kuamua kupanua mchuano huo ili kuimarisha ushindani.
4 - Taifa lililofanikiwa zaidi katika mashindano hayo ni
Misri ikiwa na mataji saba ,ikifuatiwa na Cameroon {5} Ghana {4} Nigeria {3} ,
DR Congo na Ivory Coast {2 kila mmoja wao}
5 - Madagascar, Burundi na Mauritania zitakuwa zikishiriki
kwa mara ya kwanza katika dimba hilo la 2019. Timu 12 hazajiwahi kufuzu katika
kinyang'anyiro hicho , ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya kati CAR, Chad Comoros,
Djibouti, Eritrea, Eswatini, Gambia, Lesotho, São Tomé and Príncipe,
Seychelles, Somalia na Sudan Kusini.
6 - Mshambuliaji wa Cameroon Samuel Eto'o anaongoza kwa
wingi wa magoli, baada ya kufunga magoli 18 katika michuano 18 kati ya mwaka
2000 hadi 2010.
7 - Kipa wa Misri Essam el Hadary ndiye mchezaji mwenye umri
mkubwa akiwa na miaka 44 na siku 21 kushiriki katika mchunao huo wakati
alipocheza dhidi ya Cameroon 2017 mjini Libreville.
8 - Shiva N'zigou wa Gabon ndio mchezaji wa umri mdogo zaidi
kushiriki na kufunga katika michuano hiyo. Alikuwa na umri wa miaka 16 na siku
93 wakati aliposhiriki katika michuano ya Afcon ya 2000 akifunga katika kichapo
cha 1-3 dhidi ya Afrika Kusini
9 - Mchuano huo umebadilishwa siku zake za kufanyika ili
kuzuia kugongana na kombe la dunia. Afcon kwa mara ya kwanza mwaka huu
itafanyika katikati ya mwaka kinyume na ilivyokuwa awali ambapo ilikuwa
ikifanyika mwezi Januari ili kuzuia mgongano wa mataifa na klabu za Yuropa.
10 - Mataji matatu tofauti yamekabidhiwa washindi katika
historia ya mchunao huo. Kombe la sasa lilikabidhiwa 2002 na Misri iliibuka
mshindi wakati huo baada ya kukamilisha ushindi wao wa mataji matatu 2010.
0 Comments