Yangayapigwa faini Sh milioni 2
KLABU yaYanga imepigwa faini ya Sh milioni 2 katika makosa mawili tofauti yanayouhusumichezo miwili ya Ligi Kuu.
Kosa lakwanza ambalo faini yake ni Sh milioni 1 ni mashabiki wake watatu kuonekanakwenye eneo la vyumba vya kuvalia katika mchezo dhidi ya Tanzania Prison ambaponi kinyume na taaratibu za michezo, kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF).
Taarifailiyotolewa leo Februari 15 na TFF, imeeleza kuwa adhabu hiyo imezingatiakanuni ya 17:50 na 17:60 ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.
Pia, Yangaimetozwa faini nyingine ya Sh milioni 1 kwa kosa la wachezaji wake kuchelewakurejea uwanjani katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji hali iliyosababisha mchezokuchelewa kuanza kipindi cha pili kwa dakika saba.
0 Comments