
Barcelona
imesema iko tayari kupokea ofa ya kumnunua kiungo wao wa kati Philippe
Coutinho, 26.
Manchester
United imeonesha nia ya kumsaini mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool wakati wa
msimu wa joto. (Calciomercato, via Star)
Barcelona
pia wameweka dau la pili la kumnunua winga wa Chelsea na Brazil, Willian, baada
ya ofa yao ya kwanza ya kumnunua kiungo huyo wa miaka 30 kugonga mwamba siku ya
Alhamisi. (Standard)
Chelsea
imekubali kuwanunua kwa masharti viungo wa kati Nicolo Barella, kutoka klabu ya
Cagliari na Leandro Paredes, 24, wa klabu ya Zenit St Petersburg. (Telegraph)

Meneja wa AC Milan Gennaro Gattuso amesema kuwa klabu hiyo inaendelea kuzungumza na wawakilishi wa mshambuliaji Gonzalo Higuain licha ya tetesi kuwa mshambuliaji huyo huenda akahamia Chelsea. (Express)
Kumsaini kwa
mkopo Higuain hadi mwisho wa msimu huu ndio mpango wake wakati huu wa uhamisho
wa wachezaji. (Sun)
Baba yake
Neymar ambaye ni nyota wa kamtaifa wa Brazil na Paris St-Germain amepinga uvumi
kuwa nyota huyo wa miaka 26 anataka kurejea katika klabu yake ya zamani
Barcelona. (Express)
Liverpool na
Fulham wote wanataka kumsaini mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Israel
Moanes Dabour, 26. (Estadio Deportivo - in Spanish).

Juventus
wana mpango wa kumsaini tena Paul Pogba, 25, Manchester United endapo winga wa
Brazil Douglas Costa, 28, atahamia Old Trafford kama sehemu ya mpango huo.
(Tuttosport, via Calciomercato)
Juventus pia
wako tayari kumuachilia beki wa kati wa Morocco Medhi Benatia, 31, kuenda
Arsenal katika hatua ambayo itamwezesha Aaron Ramsey, 28, kuhamia upande
wowowte. (Gazzetta dello Sport, via Metro)
Wolves
wazidi kushangaza miamba, wawalaza Liverpool
Barcelona
wanatafakari uwezekano wa kumchukua mshambulaji wa Chelsea na Uhispania Alvaro
Morata, 26 kwa mkopo.
Morata
huenda akanunuliwa na Sevilla na Atletico Madrid. (Sport - in Spanish)
Nahodha wa
Arsenal Laurent Koscielny, 33, amekataa ombi la Monaco la kutaka ajiunge nao.
(Le10 Sport, via Mirror)
chanzo BBC
0 Comments