Coastal
Union inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Juma Mgunda imeizima Mawenzi
Market Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa kuichapa 2-0, mabao ya Raizin
Hafidh dakika ya 24 na Athuman Iddi ‘Chuji’ dakika ya 72, hivyo kurejea tena
Ligi Kuu misimu miwili tangu wateremke.
Nayo KMC ya
kocha Freddy Felix Minziro imeichapa 1-0 JKT Mlale Uwanja wa Maji Maji mjini
Songea, bao pekee la kiungo Abdulhalim Humud ‘Gaucho’.
Wachezaji wa
Coastal Union wakimpongeza Raizin Hafidh baada ya kufunga bao la kwanza dakika
ya 24 leo Uwanja wa Jamhuri
Matokeo ya
mechi nyingine za leo Polisi Tanzania imeshinda 2-1 dhidi ya wenyeji Mufindi,
Mbeya Kwanza imewatandika 3-1 Polisi Dar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na
kuwateremsha hadi Daraja la Pili.
Baada ya
matokeo hayo, KMC inamaliza kileleni mwa Kundi B kwa pointi zake 28, ikifuatiwa
na Coastal Union pointi 26, JKT Mlale pointi 25, Polisi Tanzania pointi 24,
Mbeya Kwanza pointi 22, Mufindi pointi 13, Mawenzi pointi nane na Polisi Dar
pointi tano.
Ikumbukwe,
JKT Tanzania, zamani JKT Ruvu imekwishapanda kutoka Kundi A na baada ya mechi
za leo itajulikana timu nyingine ya kundi hilo ya kupanda.
0 Comments