Raia wa
Ujerumani Gerd Winkdl (60), amefariki dunia Zanzibar akidaiwa kuchomwa kisu na
marafiki zake wa kike kutokana na wivu wa kimapenzi huku wanawake wanne
wakishikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na kifo hicho.
Tukio hilo
lilitokea usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya Shangani Mkoa wa Mjini Magharibi,
Unguja.
Kamanda wa
Polisi wa mkoa huo, Hassan Nassir Ali, alisema tukio hilo lilitokea majira ya
saa 9:30 usiku baada ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2018 akiwa na marafiki zake
hao.
Alisema
kabla ya kukutwa na umauti, Winkdl akiwa na marafiki zake wanne ambao wanadaiwa
kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi, waligombana na baadaye ugomvi huo
kusababisha kuchomwa kisu katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda Ali
alisema watuhumiwa hao wanne ambao wote ni wanawake, raia wa Tanzania na Jeshi
la Polisi linaendelea kuwashikiliwa kwa ajili ya kuwahoji na kukamilisha
taratibu za kiuchunguzi.
"Inasemekana
wote walikuwa wameshalewa na inadaiwa kuwa chanzo cha ugomvi ni wivu wa
kimapenzi, lakini tunaendelea na uchunguzi," Kamanda huyo alisema.
Aidha,
Kamanda Ali alibainisha kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospitali ya
Mnazimmoja kisiwani hapa.
Aliongeza
kuwa raia huyo wa kigeni alikuwa anaishi Zanzibar akiwa ni msimamizi wa mapishi
katika hoteli moja ya kitalii kisiwani hapa.
0 Comments