Rais wa
Marekani Donald Trump ametishia kukata msaada wa kifedha kwa serikali ya
Palestina, kwa maelezo kwamba Marekani inawalipa mamia ya mamilioni ya dola za
kimarekani kwa mwaka na hakuna chochote inachoambulia , hakuna cha shukrani ama
heshima kutoka kwa taifa hilo.
Katika
utamaduni aliojijengea rais wa Marekani ,Donald Trump wa utumizi wa mtandao wa
kijamii wa twitter kama sehemu yake ya kutolea matamko , rais amesema kwamba
Wapalestina hawana mpango wowote wa kuwa na mazungumzo ya maridhiano na amani
na Israel na kuhoji uhalali wa Marekani kuendelea kujitoa kwa kiasi hicho.
Mwezi
uliopita rais wa Palestina Mahmoud Abbas alitoa tamko la taifa lake kutokuwa
tayari kupokea mpango wowote wa amani kutoka Marekani, baada ya mji wa
Washington kuitambua Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli.
0 Comments