Viongozi 17
wa ACT- WAZALENDO na 19 wa CHADEMA wa ngazi mbalimbali wakiwemo wajumbe wa
Kamati kuu, Wenyeviti na Makatibu wa mikoa, wilaya na kata kutoka mikoa
mbalimbali wamevihama vyama vyao na kujiunga na CCM tarehe 17 Januari 2018
katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro. Viongozi hao
wamepokelewa na Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu
Humphrey Polepole.
Maamuzi ya
viongozi hao yametokana na kile wanachodai kuwa vyama vyao vimehama kutoka kuwa
taasisi za umma na kuwa kampuni za watu binafsi na wapambe wao, aidha, viongozi
hao wamekiri kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Awamu ya Tano na wameguswa na Mageuzi makubwa yanayofanywa na Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kipindi hiki.
Mmoja wa
viongozi hao, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo, Ndugu
Kansa Mohammed Mbaruku amefafanua kuwa maamuzi hayo ya kukihama chama cha ACT
na kujiunga na CCM ni kutokana kuwepo na ugonjwa mkubwa sana uliyopo kwenye
vyama vya upinzani, wa kutokutembea kwenye maneno na misingi yake, vinasema ni
vyama vya kidemokrasia ila havina demokrasia kabisa na mambo mengi yanakwenda
kinyume na misingi ya uanzishwaji wa vyama hivi na jambo hili linawakatisha
tamaa wanachama wengi wa vyama hivi
Akizungumza
kwa niaba ya wanachama wa Chadema waliohamia CCM, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa
Wilaya ya Siha, Ndg. Daniel Nkini amesema wamegundua Chama cha Mapinduzi katika
masuala ya maendeleo hakibagui wananchi tofauti na ambavyo vyama vingine
vimekuwa vikitenda.
Katibu wa
Itikadi na Uenezi ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi amewapokea viongozi hao
waliokuwa wa vyama vya upinzani, amewahakikishia wamefanya uamuzi sahihi,
wamechagua upande mzuri na washirikiane na wanachama wengine wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kukijenga chama na nchi ya Tanzania.
Ndugu
Polepole amewaapisha wanachama hao, Katika kiapo cha Imani na Ahadi za
mwanachama wa CCM na akisisitiza umuhimu wa wanachama wapya na wale wazamani
kujengeka kiitikadi na kiimani ya Chama na kuishi sawasawa na Imani, Itikadi na
Ahadi za mwana CCM huku akinukuu usemi maarufu wa “Imani bila matendo imekufa”.
Huu ni
muendelezo wa mamilioni ya watanzania wanaojiunga na CCM na mamia ya viongozi
wa vyama vya upinzani kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika awamu hii ya
tano chini ya uongozi wa Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa
na,
IDARA YA
ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA
MAPINDUZI (CCM)
MOSHI,
KILIMANJARO
0 Comments