Tajiri na
Mfanyabiashara mkubwa duniani, Bill Gates amemuonya rais wa Marekani Donald
Trump kwa misimamo ya sera yake ya “Marekani Kwanza” kuwa inaweza kuharibu
uhusiano wa nchi hiyo na bara la Afrika.
Ameyasema
hayo katika mkutano wa dunia wa uchumi World Economic Forum (WEF) unaofanyika
huko Davos nchini Switzerland ambapo amesema kuwa kunatakiwa kuwepo kwa uwiano
wa wenye nguvu kubwa na nguvu kidogo.
Amesema kuwa
Marekani inaweza kupoteza ushawishi wake barani Afrika huku nchi kama China
zinazidi kuimarisha uhusiano na bara hilo kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Bill Gates
anamfuko wake barani Afrika unaoitwa Bill & Melinda Gates Foundation, ambao
umekuwa ukijihusisha kwa kiasi kikubwa kutoa huduma za afya katika nchi kadhaa.
Hata hivyo,
Rais Trump amesema kuwa atakata msaada wa bajeti ya afya kwa takribani dola bilioni
2.2 katika mfuko wa dunia, huku akiwakasirisha viongozi wa Afrika bada ya
kuyaita mataifa ya Afrika machafu kupindukia.
0 Comments