Aliyekuwa
Mbunge Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia ambaye amehamia CCM ametangaza nia ya
kugombea tena ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya chama hicho tawala.
Desemba 2
Mtulia alijiuzulu nafasi ya ubunge, huku akisema amefikia uamuzi huo bila
kushawishiwa mtu yeyote na amebaini Serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya
kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani iliahidi
kuyatekeleza.
Baada ya
hatua hiyo, chama cha CUF upande wa Profesa Ibrahim Lipumba kilitangaza
kuwaomba radhi wapiga kura wa Kinondoni kwa Mtulia kujiuzulu uanachama kisha
ubunge.
Lakini jana
Jumanne Desemba 19, 2017 kupitia andiko lake mtandaoni, Mtulia amesema
atachukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa ndani ya CCM ili agombee tena
nafasi hiyo.
"Kwaza,
nawasalimu wote na khasa wananchi wenzangu wa jimbo la Kinondoni. Nawapa pole
sana kwa maumivu makali mliyoyapata kutokana na uamuzi wangu wa kujiuzulu
ubunge wa jimbo letu la Kinondoni kupitia chama cha CUF. Nawahakikishia kwamba
bado nawapenda sana na niko tayari kuwatumikia tena kwa lengo la kuleta
Maendeleo kwenye jimbo letu" aliandika Mtulia Mtulia alitumia nafasi hiyo
kutangaza nia yake kutaka kugombea; "Nichukie fursa hii kutangaza nia kwa
wanakinondoni wote na Watanzania kwa ujumla kuwa nitachukua form ya kuomba
ridhaa kwenye chama changu cha CCM na endapo chama changu kitaridhia basi
nitakuja mbele yenu kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya ubunge wa
jimbo letu Kinondoni" Kufuatia ujumbe huo ndipo hapo baadhi ya wananchi
walianza kumpa maneno wakionyesha hisia zao juu ya jambo alilofanya na
analotaka kulifanya.
0 Comments