Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) amesikika
asubuhi hii wakati akihojiwa na Radio Clouds Fm kwenye kipindi cha Power
Breakfast, akisema kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimechukua
fomu za kugombea ubunge katika uchaguzi wa marudio Jimbo la Singida Mashariki,
mkoani Singida.
Kupitia taarifa hii ya awali, tungependa vyombo vya habari
na umma kwa ujumla ujue kuwa;
1. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakijateua
mgombea kuwania nafasi ya ubunge katika uchaguzi huo wa marudio, Jimbo la
Singida Kaskazini.
2. Mkurugenzi wa NEC, Ndugu Ramadhan Kailima atambue kuwa
suala la kugombea nafasi ya ubunge kwa mchakato wa ndani ya CHADEMA
linasimamiwa na Kamati Kuu ya Chama na hivyo hivyo yeye hana mamlaka wala
hawezi kuwa msemaji wa suala hilo katika hatua ya sasa.
3. Tunafuatilia kupata taarifa za kina kuhusu msingi wa
kauli ya Mkurugenzi hiyo, kisha tutatoa taarifa kamili katika hatua ya baadae.
Imetolewa leo Jumanne, Desemba 19, 2017 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
0 Comments