Msanii wa
nyimbo za Injili aliyetamba kwa vibao vyake murua na vyenye kuburudisha Rose
Muhando, ametangaza kujunga rasmi na Chama cha Mapinduzi.
Msanii huyo
ambaye aliomba kujiunga na chama hicho amekabidhiwa kadi ya Chama cha Mapinduzi
leo yeye pamoja na kikundi chake, katika Mkutano Mkuu Maalum wa Tisa wa CCM
Taifa, unaofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, mjini Dodoma.
Rose Muhando
kabla ya kukabidhiwa kadi ya chama cha CCM alitumbuiza kwa kibao maalumu
alichokiandaa kwa ajili ya Rais John Pombe Magufuli ambacho amekipa jina la
“Magufuli Tubebe”.
Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey polepole alitangaza kuwa Rose Muhando pamoja
na Kundi lake wameomba kupewa nafasi ya kutumbuiza kwa wimbo huo maalumu pamoja
na kukabidhiwa kadi za CCM.
“Kundi la
Ndugu Rose Muhando na yeye mwenyewe niwakaribishe Jukwani kwa wimbo ambao
wameutunga maalumu kwa Ndugu Magufuli. Kundi hili walipokuwa wanakuja walikuwa
na maombi mawili, ombi la kwanza ni kupewa nafasi ya kuimba wimbo huu maalumu
na pili kujiunga rasmi na CCM,” amesema katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey
Polepole.
Hata hivyo
Polepole amesema kuwa Rose Muhando na kundi lake watakabidhiwa kwa makatibu wa
mikoa husika kwa ajili ya michakato ya kuwaandikisha kama wanachama wapya wa
CCM.
0 Comments