Katibu mkuu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana leo ameteuliwa na Mwenyekiti
wa Chama hicho, Rais John Pombe Magufuli kuendelea kuwa katika nafasi yake kwa
kipindi kingine.
Akiongea
katika mkutano wa 9 wa Chama hicho unaoendelea mkoani Dodoma amemshukuru kwa
kazi yake nzuri kwa muda wote ambao amekuwa katika nafasi hiyo huku akiweka
wazi kuwa ni lazima aendelee kufanya nay kazi kwasababu ameridhishwa na
utendaji wake wa kazi.
''Namshukuru
ndugu Kinana kwa msaada wake mkubwa alionipa kwa kipindi chote hicho nafikiri
anafaa kuendelea kuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi kingine,'' amesema
Magufuli.
Kauli ya
Rais Magufuli inaondoa tetesi zote zilizokuwa zinadai kuwa Kinana ameandika
barua ya kuomba kujiudhuru katika nafasi yake kwa kilichodaiwa kuwa haridhishwi
na utendaji wa Mwenyekiti wake Rais Magufuli.
Baada ya
kupata nafasi hiyo Abdulrahman Kinana amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini
pamoja na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kukijenga chama hicho
pamoja na nchi kwa ujumla.
Kinana
aliwahi kuwa mtumishi wa Jeshi la Tanzania kwa miaka 20 pamoja na kuwa Spika wa
kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001 hadi 2006, amechaguliwa kuwa
Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), tangu 2012.
0 Comments