Katibu wa
itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Humphrey Polepole amevipiga
kijembe vyama vya upinzani akimtaka mwenyekiti wa moja ya vyama hivyo kusema
hela ziko wapi.
Kupitia
ukurasa wake wa “Twitter” Polepole amendika maneno hayo bila kufafanua ni
mwenyekiti wa chama gani na hela za nini japo wafuasi wake wengi katika mtandao
huo wamechangia mawazo wakitaja huenda ni hela za ruzuku.
Mbali na hilo
Polepole pia amesema kuwa kile alichowahi kukitabiri kuwa upinzani hawataweza
kushindana na chama chake siku za baadaye kimeanza kutimia.
Hii
inatafsiriwa kama majibu kwa mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freman Mbowe ambaye hivi
karibuni alitangaza chama chake hakitashiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge endapo
Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) haitazifanyia kazi kasoro zilizojitokeza kwenye
uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika mwezi Novemba mwaka huu.
“Nalipata
kuwaambia wataweka mpira kwapani, wakasubiri siku kadhaa na hatimaye imekuwa.
Kwa lugha ya shule ya msingi miaka ile ningesema "wameogopa kuputa",
wangeputa waone namna ambavyo kwetu siasa za masuala zinalipa. Ushauri wangu:
"Mwenyekiti" lazima aseme hela ziko wapi”, ameandika Polepole.
0 Comments