Tume ya
Taifa ya Uchaguzi imeeleza kuwa inawashangaa viongozi wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) wanaosema kuwa hawamtambui mgombea wa ubunge aliyesimamishwa
kugombea katika jimbo la Singida Kaskazini.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima ameeleza kuwa
CHADEMA kupitia Katibu wa Wilaya wa Singida Vijijini wamekamilisha mchakato wa
utambulisho wa mgombea wa Ubunge jimbo la Singida Kaskazini, Joseph Njumbe
“Halmashauri
ya Wilaya ya singida wagombea 6 wameteuliwa juzi mmojawapo akiwa bwana Joseph
Njumbe wa CHADEAMA. Ameteuliwa kwa sababu amekidhi vigezo vya kikatiba,
kisheria na kikanuni yeye na chama chake cha Demokrasia na Maendeleo.”
“Kwa hiyo
wanapolalamika kwamba huyu hawamjui nawashangaa sana. Nawashangaa sana kwa
saababu Kwa mujibu wa ibara ya 67 ibara ndogo ya 1b ya katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inasema Mgombea yeyote wa ubunge lazima awe amependekezwa
na chama cha siasa kilichosajiliwa.”
“Kanuni
namba 31 kanuni ndogo ya kwanza ya uchaguzi wa Rais na wabunge ya mwaka 2015,
inasema mtu akitaka kugombea ubunge atawasilisha barua yake ya utambulisho
iliyosainiwa na katibu wa chama au wa wilaya wa chama husika. Barua yake
inawasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi.”
“Huyu Bwana
David Joseph Njunbe amewasilisha barua hiyo ya utambulisho iliyosainiwa na
katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Singida Vijijini, Bwana Amani M mloya,” amesema
Kailima.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi NEC, Kailima Ramadhani amesema kuwa kwa kupitia kanuni na vigezo
vya sheria ya uchaguzi, Mgombea huyo wa CHADEMA amekidhi vigezo vyote
vilivyohitajika ili kupitishwa kugombea Ubunge katika jimbo hilo.
Aidha,
Kailima ameeleza kuwa Joseph Njumbe, pamoja na kuwa ameshakamilisha taratibu za
kupitishwa kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, bado ana haki ya
kikatiba ya kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho pale tu atakapotimiza
taratibu zinazotakiwa ili kujiondoa.
Kailima
aliongeza kuwa Tume ya Uchaguzi haiangalii
“Sisi
hatuangalii muhtasari wa kamati kuu ama hatuangalii katiba iliyosajiliwa na
Katibu Mkuu wa chama chochote cha siasa. Tunaangalia barua iliyosainiwa na
Katibu wa Chama wa Mkoa ama Katibu wa Chama wa Wilaya na ni kwa mujibu wa
sheria, kanuni na maelekezo,” amesema Kailima.
CHADEMA
pamoja na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)
vilitangaza kutokushiriki uchaguzi huo mdogo wa wabunge na madiwani
unaotarajiwa kufanyika Januari 18, 2018 ikidai kuwa mwenendo wa hali ya kisiasa
nchini siyo shwari na kuitaka Tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi huo.
Juzi CHADEMA
kupitia Mkuu wake wa Idara ya Mawasiliano, Tumaini Makene ilitoa taarifa kuwa
hakijateua mgombea wa ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini na kumtaka
Ndugu. Ramadhani Kailima kutambua kwamba mchakato wa uteuzi wa mgombea wa
ubunge ndani ya CHADEMA linasimamiwa na Kamati kuu ya Chama hicho.
0 Comments