
Mbunge wa
Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC
mjini Moshi baada ya kuvunjika mkono.
Mbatia
ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
amevunjika mkono wa kushoto baada ya kuteleza na kuanguka na amelazwa katika
wodi za watu mashuhuri (VIP).
Msaidizi wa
mbunge huyo, Hamis Hamis alisema jana Jumatano Desemba 20,2017 kuwa tukio hilo
lilitokea juzi saa 2:45 usiku wakati akiondoka hotelini kurejea nyumbani.
Hamis
alisema Mbatia alikuwa akishuka ngazi katika hoteli ya Uhuru iliyopo eneo la
Shanty Town ndipo alipoteleza na kuanguka.

“Bahati
nzuri pale kulikuwa na daktari wa KCMC anaitwa Ansbert Sweetbert ndiye alitoa
huduma ya kwanza hadi kumpeleka KCMC,” alisema.
Alisema,
“Kwa kweli huyo daktari alikuwa msaada mkubwa. Ndiye aliyempeleka KCMC na
alikaa naye hadi saa nane usiku. Wauguzi na madaktari KCMC walimpa msaada
mkubwa.”
0 Comments