
Mwenyekiti
wa Chadema Wilaya ya Siha ambaye pia ni diwani wa Gararagua, Zakaria Lukumay
amejiuzulu uanachama wa (Chadema) na kujiunga na CCM.
Lukumay
ametangaza kujiuzulu siku kadhaa baada ya aliyekuwa mbunge wa Siha (Chadema), Dk
Godwin Mollel kujivua ubunge na kujiunga na CCM.
Sawa na Dk
Mollel, diwani huyo amesema uamuzi wake unatokana na kumuunga mkono Rais John
Magufuli katika kutetea na kulinda rasilimali za Taifa.
Katika barua
kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha inayoonyesha iliandikwa Desemba
24,2017 Lukumay amesema anajiunga na CCM kwa sababu ndicho chama kinachogusa
mahitaji ya Watanzania wote.
Aliyekuwa
diwani wa Chadema wa Donyomurwak wilayani Siha, Lwite Ndossi maarufu Nsonuu
Desemba 19,2017 alijivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM.
Taarifa
iliyotolewa na idara ya itikadi na uenezi ya CCM Desemba 19,2017 ilisema Ndossi
alieleza sababu za kujiunga na CCM ni kuwa amejiunga na watu wanaofanya siasa
za kufanya kazi za maendeleo na si kulumbana na maneno matupu.

0 Comments