Mbunge wa
Chadema, Upendo Peneza amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya mbunge
huyo kuitisha mkutano na waandishi wa habari bila kueleza atakachozungumza na
wengi wameanza kutabiri huenda na yeye akatangaza maamuzi magumu ya kukihama
chama hicho.
Peneza
mbunge kutoka Mkoa wa Geita ameitisha mkutano huo kipindi ambacho kumekuwa na
vuguvugu la wabunge kukikimbia chama hicho na kujiunga na CCM.
Mkutano huo
umeitisha ikiwa ni siku moja kupita tangu mbunge wa Siha wa Chadema, Dk Godwin
Mollel alipotangaza kuhamia CCM akiunga jitihada za Rais John Magufuli.
0 Comments