Follow us

Kanisa Anglikana lapata mrithi wa Askofu Mokiwa

Tangazo

Mchungaji Jackson Sosthenes amechaguliwa kuwa askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam kwa kura 110 kati ya 185 zilizopigwa na wajumbe wa sinodi wa kanisa hilo.
Mchungaji Sosthenes amemshinda Mchungani Patrick Bendera aliyepata kura 74, huku moja ikiharibika.
Uchaguzi huo umefanyika leo Jumamosi Desemba 23,2017 katika Kanisa Kuu la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam la Mtakatifu Albano lililopo Posta wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
Ofisa habari wa dayosisi hiyo, Yohana Sanga amesema uchaguzi umelenga kumpata askofu wa tano wa Dayosisi ya Dar es Salaam anayechukua nafasi ya Dk Valentino Mokiwa.
Amesema walioshiriki uchaguzi huo ni wajumbe wa sinodi ambao ni mapadri, mashemasi, walei, wajumbe wa vikao vya sinodi na wa idara katika dayosisi.

"Baada ya Dk Mokiwa kuamriwa kujiuzulu nafasi hii ilishikiliwa na kasisi mkuu, Jerome Napera ambaye leo amemkabidhi Canon Sosthenes,” amesema.

Post a Comment

0 Comments