Aliyekuwa
nyota wa soka, George Weah, ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa marudio wa urais
uliofanyika nchini Liberia.
Tume ya
uchaguzi ya nchi hiyo ilisema kwamba Weah alipata asili mia 61.5 ya kura zote zilizopigwa
na kupata ushindi kwenye kaunti 14 kati ya 15.
Weah, mwenye
umri wa miaka 51, alikuwa anashindana na makamu wa rais Joseph Boakai, kila
mmoja akitaka kujaza nafasi ya rais Ellen Johnson Sirleaf, ambaye anaondoka
mamlakani baada ya mihula miwili inayoruhusiwa na katiba ya Liberia.
Sirleaf
alimshinda Weah kwenye uchaguzi wa mwaka 2005, baada ya nchi hiyo ya Afrika
Magharibi kuibuka kutoka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Tume ya
uchaguzi ilisema asilimia 56 ya wapiga kura walijitokeza, ambao ni wachache
kuliko waliojitokeza tarehe 10 mwezi Oktoba, wakati wa duru ya kwanza ya
uchaguzi huo.
Waangalizi
walisema kwamba vituo vya kupigia kura wiki hii vilikuwa na utaratibu mzuri
kuliko uchaguzi wa oktoba.
Mgombea
mwenza wa Weah, Jewel Howard Taylor, ni mke wa zamani wa aliyekuwa rais wa
Liberia Charles Taylor, aliyeanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo
na ambaye anatumikia kifungo cha miaka 50 nchini Uingereza kwa majukumu yake
katika ukatili uliotokea nchini Sierra Leone.
Weah alikuwa
mwanasoka mwenye umaarufu mkubwa mnamo miaka ya 90. Alichezea timu kama vile
Chelsea, Manchester City na AC milan.
0 Comments