MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mwekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
Mohamed Shein amewataka viongozi wa chama kutosita kuwajadili wanachama ambao
wanakiuka maadili ya chama hususan vitendo vya rushwa.
Pia, amesema
wanachama hao wakishajadiliwa hawatasita kufukuzwa ndani ya CCM na kwamba
imefikia hatua baadhi ya watu hao ambao wanafanya vitendo hivyo wanaonewa haya.
Hayo
ameyasema jana , katika sherehe za kumpongeza kuchaguliwa tena nafasi ya Makamu
Mwenyekiti, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa Mjini ,ambapo
aliwataka viongozi hao kutofumbia macho vitendo hivyo ndani ya CCM.
Katika
maongezi yake Dk.Shein aliongeza kuwa vitendo hivyo vya rushwa si jambo jipya
ndani ya CCM na kwamba inaharibu sana maadili ya chama.
“Vitendo
hivi vya rushwa ndani ya CCM si suala jipya lakini tunaoneana huruma, tunafichiana
na baadae tunalalamikiana wakati chama ni ya wanachama hivyo lazima
tushirikiane,”alisema.
Makamu
Mwenyekiti huyo Dk.Shein alisema utaratibu wa chama kinajielekeza wanachama
ambao wanakiuka maadili wanapaswa kujadiliwa kuanzia ngazi za tawi na baadae
inawasilishwa kwenye uongozi wa juu na kuchukuliwa hatua.
Alieleza
chama kipo kwa wanachama ikiwemo kwenye mashina na matawi na taratibu
zinafafanua kuwa ngazi hizo ndipo mambo hayo yanazungumzwa kwamba mwanachama
akikiuka maadili anajadiliwa kwenye tawi.
“Anajadiliwa
kwenye kamati ya tawi na shina, kamati ya jimbo, kamati ya wilaya, Halmashauri
ya wilaya ndipo wanapojadiliwa huku kwamba anafaa ama hafai hachukuliwe hatua
za kufukuzwa ama asichukuliwe,”alisema.
Makamu
Mwenyekiti huyo alisema utaratibu unaeleza kuwa baada ya kujadiliwa wanachama
hao taarifa itapelekwa kwenye ngazi za juu na kufanya maamuzi ya kumfukuza.
“Nachotaka
kueleza kuwa kazi hii ni ya wote na kwamba jukumu kubwa ni kuhakikisha CCM
inashinda mwaka 2020 msiwafiche watu ambao wanataka kuharibu chama, na kwa
kufanya hivyo ni sawa na kuwa ndumi la kuhili tunayoyasema sio
tunayoyafanya,”alisema Makamu Mwenyekiti.
Alifafanua
kuwa kazi ya siasa ya kipindi hiki lazima kuongeza kasi ambapo kuna mambo zaidi
ya kuyafanya na hata Mwenyekiti Dk.John Magufuli alisisitiza kwenye mkutano
mkuu uliofanyika Desemba 18, mwaka huu mjini Dodoma.
Mbali na
hilo, Dk.Shein aliwataka viongozi wa serikali kutambua na kuheshimu CCM
kutokana na kuwa wanafanya kazi ya utekelezaji wa chama hivyo hawanabudi
kukithamni.
Kwa upande
wake Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Dk.Abdallah Juma Saadalla(Mabodi), alisema
wanachama kutoka visiwani humo wanatarajia kusimamia vyema ibara ya tano ya
kuhakikisha CCM inashinda mwaka 2020.
Aliongeza
kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa na mawimbi makubwa sana lakini watu walioshiriki
walikuwa wanastahili.
“Bado
tunafanya juhudi za kutoa elimu kwa viongozi wa chama kuhusu suala la
kuzingatia kanuni na maadili ili kuhakikisha wanasongesha gurudu la uchaguzi wa
mwaka 2020″alisema.
Dk.Mabodi
ameeleza kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa wagombea wote ambao wamepita kwenye
uchaguzi huo asilimia kubwa wana maadili ya kutosha
0 Comments