Diwani wa
Chadema wa Donyomurwak wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, Lwite Ndossi maarufu
Nsonuu amejivua uanachama wa chama hicho.
Pia,
amejiuzuru udiwani na ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa
iliyotolewa na idara ya itikadi na uenezi ya CCM Jumanne Desemba 19,2017
imesema Ndossi ameeleza sababu za kujiunga na CCM ni kuwa kujiunga na watu
wanaofanya siasa za kufanya kazi za maendeleo na si kulumbana na maneno matupu.
0 Comments