Chuo Kikuu Huria pekee kimepewa ruhusa ya kuendelea kutoa
kozi ya Foundation iliyokuwa imesitishwa na serikali kwa wanafunzi ambao
wamekosa vigezo vya kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu baada ya mtaala wake
kuboreshwa na kupitishwa na Wizara ya Elimu.
Ruhusa hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa
leo akiwa mkoani Singida yanapofanyika Mahafali ya chuo hicho.
Ikumbukwe kuwa Mwaka 2016 Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi
Stella Manyanya alitoa katazo hilo na kusema utaratibu wa kozi ya Foundation
umefanywa na vyuo vyenyewe hivyo serikali haiwezi kuukubali mfumo wa elimu hiyo
na kwamba kama mtu anasoma kozi ya Foundation apewe cheti na kama atahitaji
kujiendeleza asafishe cheti au asome mfumo ambao utamfikisha katika shahada.
Mbali na hayo katika Mahafali hayo ambayo Waziri Mkuu ndiye
Mgeni rasmi atamtunuuku mkewe Bi Mery Shahada ya Uzamiri ya Elimu.
"Wakati najiandaa kuja kwenye sherehe mwenzangu naye
kumbe anajiandaa, nashukuru amemaliza sasa mambo nahisi yataenda vizuri maana
wakati mambo ya masomo yalipokuwa busy hata tulikuwa hatuonani...Leo pia naona
familia yangu nayo itakuwa inasherehekea" Majaliwa
0 Comments