Mwanamuziki
na Muigizaji nchini, Patcho Mwamba ameifungukia kauli ya Mama Kanumba ya
kushukuru kitendo cha Muigizaji Lulu kufungwa miaka miwili kwa kosa la kumuua
bila kukusudia muigizaji Kanumba na kusema kwamba hakuna haja ya kuendelea na
'beef' kwani hakuna haki inayoweza kumrudisha Kanumba hai.
Patcho
ambaye alikuwa muigizaji na rafiki wa karibu na Marehemu Steven Kanumba amesema
kwamba Mama kanumba anapaswa kuwa na moyo wa kusamehe kwa sababu binti huyo
akimaliza kifungo atarudi mtaani na ataendelea na maisha yake hivyo kujengeana
chuki siyo jambo jema.
"Sina
la kusema juu ya jukumu ya Lulu, lakini Mahakama imeamua kama ilivyoamua, kwa
upande mmoja kuna unafuu kwani kwa kesi ile kufungwa miaka miwili ni bahati,
ukija upande wa pili inaumiza sana kwani jela siyo sehemu nzuri sana kwa mtu
kuwepo kila mtu anajua hilo hasa ukizingatia bado ni mdogo hivyo tumuombee
Mungu ampe nguvu, uwezo naamsaidie aweze kustahimili hiyo hali" Patcho.
Aidha Patcho
ameongeza "Nimemuona mama anasema anashukuru (Mama Kanumba) haki imetendeka,
mimi sidhani kama kunahitajika kuwepo na ma Beef. Mwanaye, ambaye pia ni rafiki
yetu ameondoka lakini tunaamini ni mipango ya Mungu. Hakuna haki inayoweza
kumrudisha Kanumba aishi. kusema naenda kumzika Kanumba upya sidhani kama kuna
haja ya kuendeleza ma beef japo yapo. End of the day Lulu atatoka wataongea
vizuri?. Sidhani yule mama yangu hivyo simshauri aendee kuwa na kinyongo".
Patcho
amemalizia na kusema kwamba "Kusema kufungwa kwa Lulu kutampatia unafuu
sidhani ni uongo yeye aendelee kuwa mama maana ninachoamini Lulu hakumuua
Kanumba bali alikuwa shahidi wakati Kanumba anakufa ndichi ninachokiamini.
Baadaye Lulu atatoka jela je ukimuon utamgonga na gari? au Mama Lulu utaweza
kuongea naye na wale ni Wahaya ni kabila moja. Sidhani kama Lulu alikuwa akikaa
na kufikiria ipo siku atamuua Kanumba".
0 Comments