Shirika la
Ndege la Coastal (Coastal Aviation) katika taarifa yake kuhusu ajali ya ndege
iliyotokea jana asubuhi limesema kuwa watu wote 11 waliokuwa katika ndege hiyo
wamefariki dunia.
Coastal
wameeleza kuwa, ndege yao, Cessna Caravan ilipata ajali majira ya saa 5 asubuhi
kwa saa za Afrika Mashariki katika eneo la Empakaai, Ngorongoro ikiwa na rubani
mmoja na abiria 11 wakati ikiwa safarini kuelekea Serengeti.
Shirika hilo
limesema kuwa majina ya waliofariki katika ajali hiyo bado hayajawekwa wazi
wakisubiria kuwajulisha ndugu zao.
Mkurugenzi
Mkuu wa Coastal, Julian Edmunds amesema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha sana,
na kwamba mara kadhaa amekuwa akisafiri na ndege za shirikia hilo na hivyo
anaimani na marubani pamoja na ndege zao.
Aidha,
ameeleza kuwa kwa niaba ya shirikia hilo na wafanyakazi wake, watafanya kila
litakalowezekana ndani ya uwezo wao kusaidia katika uchunguzi wa ajali hiyo
kwani hakuna kitu cha umuhimu kwao zaidi ya usalama wa abiria.
Kwa sasa
wameeleza kwamba wanafanya uchunguzi katika eneo la tukio na kuwa, taarifa
zaidi kuhusu chanzo cha ajali hiyo watazitoa mara taarifa kamili
zitakapopatikana
0 Comments