Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu
Mtoto wa
Marehemu Chacha Wangwe ambae alikua Mbunge wa Tarime, Bob Chacha Wangwe
kifungo cha
mwaka mmoja na nusu jela au kulipa faini ya Shilingi Milioni 5 baada ya
kupatikana na hatia kwenye kosa la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao
wa Facebook.Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo
amesema katika kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 6 na vielelezo
5 dhidi ya Bob ambae pia ni Mwanaharakati.Alisema kuwa Mei 7, 2016 polisi
walipata taarifa ya chapisho la Bob ambapo walianza kumfatilia na kumkamata
kisha walichukua simu na kuipeleka maabara ya Polisi ili kuikagua.“Kimsingi Bob
hukupinga kuandika maneno hayo lakini umedai kuwa hukuyachapisha katika jamii
bali yalikuwa ni siri kwenye akaunti yako“.Hakimu Shaidi alisema kuwa wakati wa
ushahidi simu yake ilipokaguliwa ilionekana ilitumika kuchapisha ujumbe huo kwa
jamii na watu walimjibu, ikiashiria ujumbe uliwafikia.“Hivyo ni dhahiri ulikuwa
na nia ya kuchapisha taarifa hiyo, kueleza kile ambacho ulikiona sahihi kama
ingekuwa ni ujumbe wako binafsi basi Polisi wasingeweza kukutafuta na watu
wasingekujibu“Hakimu Shahidi amesema kutokana na hatua hiyo Bob amekutwa na
hatia chini ya kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015
ambapo katika utetezi wake, Bob aliomba apunguziwe adhabu kwa sababu ni
Mwanafunzi wa masomo ya Sheria na pia ni kijana mdogo na ni kosa lake la kwanza
kulitenda.Hakimu Shaidi alisema anakubaliana na hoja za Bob kwani Mahakama
inamuona bado ni mdogo na anapaswa kufanya mambo mengi mazuri katika jamii
ambapo pia amesema kama yeye ni mwanafunzi wa masomo ya sheria anapaswa kufanya
mambo mema katika jamii vitu ambavyo wengine watamuiga.“Hivyo Mahakama
inakuhukumu kulipa faini ya Sh.milioni 5 ama uende jela mwaka mmoja na nusu na
pia milango ya dhamana ipo wazi“Katika kesi hiyo namba 167, Chacha Wange
anatuhumiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa
mtandao wa Facebook March 15,2016 ambapo aliandika maneno yafuatayo hapa
chini.“….Tanzania ni ambayo inajaza chuki wananchi.… matokeo ya kubaka
Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya Muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya
Zanzibar kuwa koloni la Tanzania Bara kwasababu za kijinga.”
0 Comments