Waziri mkuu
wa zamani, Edward Lowassa amemtumia ‘salamu’ Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kwamba gharama za kuandaa Katiba Mpya si kubwa ukilinganisha na mahitaji ya
Watanzania.
Akihutubia
mamia ya watu katika viwanja vya Soko Kuu la Kwa Mromboo jijini Arusha juzi,
Lowassa alimsihi Rais John Magufuli kuruhusu mjadala wa Katiba Mpya kwa kuwa
ndiyo kiu ya Watanzania kwa sasa.
“Wananchi
wamesema Rais Magufuli aruhusu mjadala wa Katiba Mpya, lakini waziri mkuu wake
amesema ni gharama sana mimi nasema gharama hizo ukilinganisha na idadi ya watu
wanaohitaji jambo hili ni kubwa sana atukubalie tujadili Katiba Mpya,” alisema
Lowassa huku akishangiliwa.
Baadhi ya
wabunge waliohudhuria mkutano huo ni Godblesss Lema (Arusha Mjini), Joshua
Nassari (Arumeru Mashariki) na meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro.
Lowassa,
awali aliwauliza wananchi: “Tunahitaji Katiba Mpya hatuhitaji?” na wananchi
walijibu: “Tunahitaji.”
“Mimi
pendekezo langu ni kwamba mheshimiwa Rais kwa heshima zote akubali mjadala wa
Katiba Mpya,” alisisitiza Lowassa.
Hata hivyo,
Lowassa aliwaambia watu waliohudhuria mkutano huo kuwa jambo jingine
lililomfikisha mbele yao ni kuwashukuru kwa dhati baadhi ya Watanzania
walivyompigia kura mwaka 2015, kwa sababu alizuiwa kuzunguka nchi nzima.
Awali,
mgombea udiwani wa Chadema, Simon Mollel alitaja vipambele vyake kuwa ni
kushughulikia kero za jamii hususan maji na kuwaomba wananchi wamchague.
0 Comments