
Katika
kampeni za lala salama leo, CCM itawapandisha jukwaani aliyekuwa mwenyekiti wa
Bavicha, Patrobas Katambi na Dk Louis Shika, aliyejizolea umaarufu baada ya
kuibuka kwenye mnada wa nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi.Katambi aliyejiunga
na CCM akitokea Chadema na Dk Shika watamnadi kwa wapiga kura wa Kata ya Mhandu
jijini Mwanza mgombea wake, Constantine Sima.Katibu wa uenezi wa CCM Wilaya ya
Nyamagana, Mustapha Banigwa amesema leo Jumamosi Novemba 25,2017 kuwa wengine
watakaopanda jukwaani katika mkutano utakaofanyika mtaa wa Machinjioni ni
waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi na mbunge wa Nyamagana, Lawrence
Masha aliyerejea CCM akitokea Chadema.
Mkutano huo pia utahutubiwa na mjumbe wa
Kamati Kuu ya CCM na aliyekuwa mbunge wa Bunda, Stephen Wasira, mbunge wa Nzega
Mjini, Hussein Bashe na mbunge wa Bukombe, Doto Biteko.Uchaguzi mdogo wa
udiwani katika kata 43 nchini utafanyika kesho Jumapili Novemba 26,2017.
0 Comments